Tuesday , 30 April 2024
Habari za SiasaTangulizi

Ni hofu, woga THRDC?

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Spread the love

MTANDAO wa Utetezi wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition -THRDC), hatimaye umetangaza kusitisha shughuli zake kwa muda usiojulikana. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wake wa bodi, Vick Mtetema, imeeleza shirika hilo limelazimika kufunga shughuli zake, kufuatia serikali kuzifungia akanti zake za benki na kuliweka shirika “kwenye uchunguzi.”

Amesema, “tarehe 14 Agosti 2020, mtandao ulipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau wetu, tunaofanya nao kazi, wakidai kushindwa kupata malipo yao kupitia akaunti yetu ya benki, iliyopo katika benki ya CRDB.

“Tulipofuatilia suala hili, uongozi wa benki ya CRDB ulitufahamisha kuwa wameekelezwa kufanya hivyo na Jeshi la Polisi.”

Kwa mujibu wa Mtetema, shirika lake lilifanya juhudi za kuwasiliana na mamlaka za polisi nchini Tanzania, ambapo jeshi hilo lilikiri kufanya hivyo.

Anaongeza, “lakini leo (jana Jumatatu), mratibu wa mtandao, Onesmo ole Ngurumwa, aliitwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwamo taasisi hiyo kutowasilisha mikataba kati yake na wafadhili, katika ofisi ya hazina na ofisi ya msajili.”

Amesema, baadaye Ngurumwa alichukuliwa maelezo na kupewa dhamana ya polisi kwa masharti ya wadhamini wawili ambao ni watumishi wa umma na kusaini bondi ya Sh. 200 milioni.

“Ndugu wanachama pamoja na wadau, baada ya mashauriano ya kina, kutokana na kikao cha dharura cha bodi ya wakurugenzi ya TRDC, tumefikia maamuzi ya kusitisha shughuli za taasisi kwa muda, huku tukiendelea kushughulikia utatatuzi wa suala hili,” ameeleza Mtetema katika taarifa yake.

Kupatikana kwa taarifa hizi, kumekuja katika kipindi ambacho taifa hilo linaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani, uliopangwa kufanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Vick Mtetema, Mwenyekiti wa Bodi ya THRDC

THRDC, pamoja na kutetea watetezi wa haki za binadamu na shughuli zao, limekuwa mstari wa mbele kukosoa uvunjifu wa haki za binadamu nchini, unaofanywa dhidi ya wanachama wao na watu wengine kwa ujumla.

Katika ripoti yake ya Aprili 2020, THRDC ilizitaja kwa kina kesi tisa za kimkakati zilizofunguliwa mwaka 2019 kama miongoni mwa vielelezo pamoja na matendo 71 dhidi ya watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania.

Miongoni mwa vitendo hivyo, ni pamoja kukamatwa kinyume cha sheria, vitisho, uminywaji wa uhuru wa kujieleza na kufunguliwa kesi inazozitaja zisizo na msingi huku baadhi ya wahusika wa vitendo hivyo, wakielezwa ni watu wasiojulikana.

Ripoti hiyo inaonesha jinsi waandishi wa habari nchini Tanzania wanavyopitia unyanyasaji mkubwa wakati wakitekeleza majukumu yao; kutozwa faini kwa vyombo vya habari bila kuzingatia taratibu, kunyang’anywa vitendea kazi na kusimamishwa au kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari.

Wadau wa THRDC

Jumla ya matukio 36 ya aina hiyo imeripotiwa, idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

Ngurumwa alisema, pia asasi za kiraia zinaonekana kuathirika pakubwa kutokana na sheria kandamizi ambazo zinatoa mamlaka makubwa kwa msajili, na kwamba katika kipindi hicho mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 158 yalifutiwa usajili kwa kile kilichotajwa kutokuzingatia masharti ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali marekebisho ya mwaka 2019.

Mtandao huo uliitaka serikali kutambua kazi za watetezi kwa kutengeneza mazingira wezeshi, kurekebisha sheria walizozitaja si rafiki katika utendaji kazi, zikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015, Sheria ya Vyombo vya Habari 2016 na Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2018 ili kustawisha utendaji kazi wa watetezi wa haki za binadamu nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!