Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kuchomwa ofisi za Chadema: Polisi waingia mtaani
Habari za Siasa

Kuchomwa ofisi za Chadema: Polisi waingia mtaani

Salumu Hamduni, Mkurugezni Mkuu wa TAKUKURU
Spread the love

WATU waliohusika na tukio la kuchoma Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, sasa wanasakwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Jeshi la Polisi Arusha limeeleza, kwamba lipo kwenye msako na uchunguzi kwa watu waliohusika na tukio hilo likieleza samani zilizokuwa kwenye ofisi hizo ziliteketea.

“Ni kweli ofisi zilivamiwa na kufayiwa uharibifu. Tunawasaka na tutawachukulia hatua,” amesema Salumu Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha.

Taarifa kutoka Arusha zinaeleza, usiku wa kuamkia tarehe 14 Agosti 2020, ofisi hizo zilishambuliwa na kuteketea kwa moto. Polisi wanasema ‘waliohusika hawajajulikana.

Kamanda Hamdan anasema, watu waliohusika wakikamatwa, sheria zitachukua mkondo wake. Ofisi hiyo ipo katika Kata ya Kimandolu, jijini humo.

Shambulizi kwenye ofisi hiyo zilisababisha hasara na uharibifu wa mali mbalimbali ikiwamo kuvunjwa kwa vioo vya madirisha sita. Bado thamani kamali ya uharibifu haijajulikana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!