WATU waliohusika na tukio la kuchoma Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, sasa wanasakwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).
Jeshi la Polisi Arusha limeeleza, kwamba lipo kwenye msako na uchunguzi kwa watu waliohusika na tukio hilo likieleza samani zilizokuwa kwenye ofisi hizo ziliteketea.
“Ni kweli ofisi zilivamiwa na kufayiwa uharibifu. Tunawasaka na tutawachukulia hatua,” amesema Salumu Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha.
Taarifa kutoka Arusha zinaeleza, usiku wa kuamkia tarehe 14 Agosti 2020, ofisi hizo zilishambuliwa na kuteketea kwa moto. Polisi wanasema ‘waliohusika hawajajulikana.
Kamanda Hamdan anasema, watu waliohusika wakikamatwa, sheria zitachukua mkondo wake. Ofisi hiyo ipo katika Kata ya Kimandolu, jijini humo.
Shambulizi kwenye ofisi hiyo zilisababisha hasara na uharibifu wa mali mbalimbali ikiwamo kuvunjwa kwa vioo vya madirisha sita. Bado thamani kamali ya uharibifu haijajulikana.
Leave a comment