Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Orodha ya wagombea ACT- Wazalendo, hii hapa
Habari za SiasaTangulizi

Orodha ya wagombea ACT- Wazalendo, hii hapa

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo. kimetangaza orodha ya wagombea 198 wa ubunge na uwakilishi, Tanzania Bara na Zanzibar.  Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Akitangaza orodha hiyo, leo Jumapili, tarehe 16 Agosti 2020, katibu mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, ametaja wagombea hao, waliopitishwa na Kamati Kuu (CC), iliyokutana juzi na jana, tarehe 15 Agosti. 

Kwa mujibu Ado, majimbo 66 yaliyosalia wagombea wake hawakuweza kupitishwa kutokana na kile alichoita, “mapingamizi yaliyowekwa na washindani wao kwenye nafasi hizo.”

Majimbo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), na ambayo yatashindaniwa kwenye uchaguzi, jumla yake, ni 264.

Alisema, “…baada ya muda mfupi hayo majina yatasomwamaana kuna masuala yanawepitiwa.”

Aidha, chama hicho kimewapitisha wanawake kadhaa kugombea uwakilishi na ubunge wa jukwaani, wakiwamo waliowahi kuwa wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la 10 na Bule lililopita.

Miongoni mwa waliopitishwa, ni Raisa Abdallha Mussa, aliyepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Mfenesini, Riziki Shahari Mngwali, aliyepitishwa kuwania nafasi hiyo katika jimbo la Mafia, mkoani Pwani na  Kulthum Jumanne Mchuchuli, aliyepitishwa kugombea nafasi hiyo, katika jimbo la Rufiji.

Ado alisema, chama chake kimempitisha aliyekuwa mbunge wa Ubunge, jijini Dar es Salaam, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ndg. Saed Kubenea, amepitishwa kugombea ubunge katika jimbo la Kinondoni; huku aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika jimbo la Ubungo, Renatus Pamba Mkonga, amepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Ubungo.

Wagombea wengine waliopitishwa na majimbo yao kwenye mabano, ni kama ifuatavyo:

Mbarala Maharagande (Segerea), Webiro Wakazi Wassira (Ukonga), Mwanaisha Zuberi Mndeme (Kigamboni), Hussein Juma Abdallah (Ilala), Moses Ndonde (Kibamba), Kondo Juma Bungo (Mbagala), Rashid Jumbe Hamza (Tanga Mjini), Faraji Msagati (Pangani), Mwajabu Athuman Dhahabu (Lushoto) na Rehema Ally Mohammed (Mkinga).

Wengine, ni Bahati Hamad Chirwa (Korogwe Mjini), Emmanuel Mnakai (Mlalo), Zitto Zuberi Kabwe (Kigoma Mjini), Swage Zahir Swage (Kigoma Kaskazini), Said Rashid Bakema (Kigoma Kusini), Hamza Jaffar Mtunu (Kasulu Mjini), Edibily Kazala Kinyoma (Kasulu Vijijini), Sendwe Ibrahim Mbarouk (Manyovu), Julius Joseph Massabo (Muhambwe), Mtondo Haruna Balele (Buyungu) na Uledi Hassan Abdallah (Mtwara Mjini).

Katika orodha hiyo, wapo pia Fuata Issa Nabaraka (Mtwara Vijijini), Mbaraka Chilumba (Newala Mjini), Dadi Rashid Chimeta (Newala Vijijini), Alphonce Andrea Hittu (Tandahimba), Mussa Mustapha Mussa (Masasi Mjini), Hamis Dadi Mwalimu (Nanyamba), Hassan Loani Namagono (Nanyumbu),  John Shayo (Arusha Mjini), Alfayo Bigoli Nebugo (Ngorongoro) na  Meshack Meliyo Laizer (Arumeru Mashariki).

Wengine, ni John Emmanuel Kivuyo Lairunge (Arumeru Magharibi), Cornel Bupolo Matinde (Misungwi), Misana Mtaki Gatawa (Ukerewe), Adams Ibrahim Chagulani (Nyamagana), Mkiwa Adam Kimwanga (Ilemela), Esau Sospeter Lushanga (Magu), Kabura K. Masibuka (Sengerema), Faustine Precide Ruhabuza (Buchosa), Bonifasia Aidan Mapunda (Namtumbo) na Ado Shaibu (Tunduru Kaskazini).

Wapo, pia Issa Jaffar Ahmad (Tunduru Kusini), Mohammed Juma Mtambo (Mkuranga), Ramadhan Mohammed Mketo (Kibiti), Amina J. Mshana (Kibaha Mjini), Vitali Mathias Maembe (Bagamoyo), Fabian Leonard Sikauki (Chalinze), Zavala Mussa Zavala Pazi (Kisarawe), Dunia Juma Dunia (Igalula), Elly Jeremiah Tunduza (Tabora Mjini),  Njile Nkuba Sitta (Kishapu) na  Soud Swaibu Katikiro (Kondoa Mjini).

Katika orodha hiyo, wapo pia Jackson Mahuma Gagu (Kondoa Vijijini), Said Salim Njuki (Kalenga), Hezron Weilus Mahembe (Kilolo) na Said Mwalimu Kiyange (Isimani), Robert Swira Haonga (Mafinga).

Soma orodha kamili hapa chini:-

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!