Friday , 1 March 2024
Habari za SiasaTangulizi

Lissu atashinda?

Spread the love

HARAKATI za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 zinashika kasi. Tayari wagombea ngazi ya urais bara na visiwani wanajulikana. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni miongoni mwao, lakini je atashinda? Hili ndio swali kuu linalotawala wengi.

Upinzani wa Lissu kwa utawala unampa mvuto pia kwa raia ambao hawaridhishwi na namna mambo yalivyoendeshwa kwa miaka mitano sasa.

Lissu anapata uungwaji mkono kutoka ndani ya chama chake na hata nje ya chama chake, anaungwa mkono na wanaharakati wanaojipambanua hisia zao na wale wasiojileleza hadharani.

Ndani ya Chadema Lissu anatajwa kama mwanasiasa jasiri, mwenye kufikisha ujumbe wake kwa jamii na watawala katika namna yake ya kipekee.

Taswira na kauli zake vinaakisi kile kilichomo kwenye ubongo wake. Ushawishi wake ndani ya chama chache (Chadema), ndio uliowasukuma wajumbe wa Baraza Kuu kumpigia kura za ushindi. Kwenye kura za maoni za urais Chadema, Lissu alishinda kwa kupata kura 405 kati ya 442.

Kwa sasa yupo mikoani kusaka wadhamini kama ilivyo kwa wagombea wa vyama vingine. Amekumbana na mengi lakini siasa zake hazijabadilika.

Mazingira ya siasa kuanzia mwaka 2015 yana utofauti mkubwa na yale kabla ya mwaka huo. Baada ya 2015, malalamiko ya vyama vya upinzani kuhusu kukosa nafasi ya kujinadi yalishamiri.

Yapo mambo kadhaa ambayo yatasababisha Lissu kuvuta masikio ya wengi. Wapiga kura wengi watamfuata, watamsikiliza na kisha kuamua kutokana na hoja zake.

Kwa miaka mitano Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake Dk. John Magufuli, walikuwa na uwanda wa kipekee wa kujieleza kwa wananchi.

Hawakupata bughudha yoyote, walikwenda kule walikotaka, walifanya walichotaka na kwa wakati walioutaka. Ni nafasi ya kipekee iliyotumika kujigamba kwa kile serikali ya CCM imekifanya.

Wananchi walikuwa wana nafasi ya kusikiliza mazuri ya serikali. Kwa kawaida, hakuna serikali iliyokosa kasoro ambazo wanasiasa huchukua hatamu ya kuzizungumza kwenye majukwa yao. Kasoro hizo hazijazungumzwa kwa uwanzi na uhuru, bila shaka uwanja huo utatumiwa na Lissu.

Sehemu kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika miaka mitano (2015-2020) ipo wazi, miradi mikubwa kwa midogo iliyotekelezwa na Serikali ya CCM inajulika kwa Watanzania.

Miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa madaraja, ununuzi wa ndege, upanuzi barabara, meli pamoja na mradi wa umeme Rufiji – Stiegler’s Gorge tayari inatawala kwenye vichwa vya wengi.

Changamoto za utekelezwaji wa miradi hiyo hazijawa wazi, wananchi hupenda kusikia pande zote, Lissu na wapinzani wengine watalazimika kueleze changamoto hizo.

Masikio ya Watanzania huhitaji kitu kipya, kunadi kilichofanywa na serikali ya CCM kwenye uchaguzi huu hakiwezi kuwa ‘ishu’ lakini kueleza changamoto za kile lilichofanywa na CCM ndio kinaweza kuwa na mvuto.

Lissu anaweza kuvuta hisia za wengi kueleza upande wa pili wa shilingi, upande huu haujazungumzwa kwa kiwango chake. Ujasiri na ushawishi wake unaweza kuvuta wengi kumsikiliza.

Lissu hakuwepo nchini kwa takriban miaka mitatu, hamu ya Tatanzania kumsikiliza akiwa jukwaani ni kubwa kuliko wagombea wengine. Wanaokwenda kumsikiliza wanatarajia kusikia vitu tofauti na vile walivyokuwa wakisikia kwa miaka mitano sasa.

Si tofauti tu kwa maana ya utofauti, hata namna ya uwasilishaji wake unaweza kuongeza mvuto na ushawishi, hivyo kumuweka katika nafasi nzuri.

Huruma. Wapo Watazania walioumizwa na kitendo cha kushambuliwa kwa risasi, kikubwa zaidi ni kutopatikana kwa watuhumiwa waliohusika kwenye shambulio hilo.

Lissu alishambuliwa kwa risasi jiji Dodoma tarehe 7 Septemba 2020. Watanzania wengi wanahitaji kujua nini kilitokea katika uhalisia wake, Lissu anaweza kutumia jukwa la kampeni kuzungumza hali halisi na mazingira yalivyo. Hili hajawahi kulifanya mbele ya umma.

Staili ya Lissu katika uzungumzaji inaweza kuwavutia vijana wengi. Baadhi ya vijana huonekana kupenda siasa za majibizano jambo ambalo mgombea huyo analiweza.

Katika mazingira hayo yaliyoandaliwa na Serikali ya CCM kwa miaka mitano, Je Lissu ataweza kushawishi Watanzania kumpigia kura? Tusubiri.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!