Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba yazindua nembo na jezi mpya
Michezo

Simba yazindua nembo na jezi mpya

Spread the love

KLABU ya Simba leo Ijumaa 14 Agosti, 2020 imezindua nembo yake mpya na jezi zitakazotumika kwenye msimu ujao wa kimashindano 2020/21 katika michuano ya ndani na nje ya nchi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Uzinduzi wa nembo hiyo pamoja na jezi uli0fanyika leo kwenye ofisi za klabu hiyo Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mwina Kaduguda na msemaji mkuu wa klabu hiyo, Haji Manara sambamba mchezaji mpya wa klabu hiyo, Benard Morrison.

Klabu hiyo imetambulisha jezi tatu huku nyekundu na nyeupe zitakuwa za nyumbani na bluu itakuwa ya ugenini.

Kwa upande wa nembo mpya ya klabu hiyo Afisa habari wa kikosi hiko, Manara amesema kuwa lengo la kufanya mabadiliko hayo ni kuendana na matakwa ya kibiashara katika soka la sasa.

“Matakwa ya sasa ya mpira na kibiashara, klabu nyingi duniani zimeamua kubadilisha nembo yake kutokana na matakwa ya kibiashara, ni klabu chache sana kubwa ambazo zimeendelea na nembo yake ileile tokea kuanzishwa kwake,” alisema Manara.

Nembo hiyo ambayo inaonekana tofauti na ile ya zamani huku kaulimbiu ya klabu hiyo ambayo ni ‘nguvu moja’ ikiwa imeondolewa lakini bado itaendelea kutumika lakini sio kukaa kama sehemu ya nembo hiyo kama ilivyokuwa hapo awali.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Kaduguda amesema kuwa, amepata bahati ya kuiona timu hiyo toka ikiitwa Sunderland na kuwa na nembo tofauti tofauti na kusema kuwa nembo hii inaonesha Simba mwenye njaa.

“Kulikuwa na nembo ya Simba yenye Simba wawili ikiwa ndio nembo ya kwanza, Nembo ya pili ilikuwa na Simba mwenye kicha na baadae Simba mzima, tukaenda nayo mpaka sasa tulipoibadilisha hii na kumuweka samba mwenye njaa,” alisema Kaduguda.

Kuzinduliwa kwa jezi na nembo hiyo kumaonesha kuwa Simba imeshaanza maandalizi rasmi kuelekea msimu ujao wa Ligi ambapo kuanzia leo wataanza kutambulisha wachezaji wapya watakao watumia kwa msimu ujao.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!