Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Tukishindwa tutakubali, lakini tukishinda…
Habari za Siasa

Maalim Seif: Tukishindwa tutakubali, lakini tukishinda…

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema, endapo watashindwa kihalali katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 watakuwa tayari kukubali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wenyewe utafanyika siku mbili kuanzia tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Maalim Seif amesema iwapo watashinda hawatakubali kufunga mikono yao nyuma.

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 wakati akifungua mkutano mkuu wa ACT-Wazalendo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Mkutano huo utakuwa na ajenda mbili za kuteua wagombea urais wa Juamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar na kupitisha Ilani ya uchaguzi mkuu.

“Tuwachague hao wagombea ambao tuna imani, wakipeperusha bendera yetu watashinda na kutekeleza yale yaliyoahidiwa katika Ilani ya ACT-Wazalendo,” amesema Maalim Seif

Maalim Seif amesema, “Miaka 59 ya utawala wa CCM, umasikini umekuwa zaidi. Wananchi wamekuwa wajinga zaidi. Maradhi yametamalaki. Wenzetu ni kujisifu tu. Lakini miaka mitano hii, hali imekuwa zaidi.”

Mwenyekiti huyo amesema, Tunakwenda katika kinyang’anyiro ambacho kila chama kina mgombea wake, “tunataka kuiona Tanzania nyingine kabisa. Tanzania inayoendelea kwa kasi kubwa. Huduma zote muhimu zinakuwa bora na hiyo ndiyo ‘vision’ ya ACT-Wazalendo.”

“Tukishirikiana na kuwauza wagombea wetu, ACT-Wazalendo itaibuka na ushindi na wanaosema hawataondoka madarakani, wahesabu siku zao, wala wasidhani mara hii chama chetu kitashinda na sisi tutafunga mikono,” amesema huku akishangiliwa

“Tukishinda kihalali tutakubali na mimi kule Zanzibar mgombea akishinda nitampa mkono lakini mara hii tumekusudia, tumeamua kulinda maamuzi ya wananchi,” amesema Maalim

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!