October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wiki hii: JPM, Lissu ‘kukutana’ NEC

Spread the love

MIOAMBA miwili ya siasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, inatarajiwa ‘kupigana kumbo’ katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC), Dodoma wakati wa kuchukua fomu za urais. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wakati Tundu Lissu, mgombea urais wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema), akitangazwa kuchukua fomu ya kugombea urais wiki hii tarehe 8 Agosti 2020, Dk. John Magufuli ndani ya waki hii atachukua fomu.

Mpaka leo, zimebaki siku tano kukamilika wiki ambapo kila mmoja anatarajiwa kufika kwenye ofisi hizo zinazotumia majengo yake mapya yaliyopo katika eneo la Njendengwa, jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 5 Agosti 2020, mbele ya waandishi wa jijini Dar es Salaam, Dk. Magufuli ambaye ni Rais wa sasa wa Tanzania, atafika kwenye ofisi za NEC kuchukua fomu ya kugombea urais, hata hivyo hajataja siku, tarehe wala muda wa tukio hilo.

            Soma zaidi:-

 

“Napenda kuwatangazia rasmi kabisa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ambaye sisi kwenye chama chetu ndio muasisi mkubwa wa uwazi, atachukua fomu wiki hii, ni lini nitawaambia tena, lakini wiki hii mgombea CCM atachukua fomu kule jijini Dodoma,” amesema Polepole.

Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, ambapo NEC imefungua zoezi la uchukuaji fomu ngazi ya urais kuanzia leo na kuhitimishwa tarehe 25 Agosti mwaka huu.

Rais Magufuli alipitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM kugombea nafasi hiyo Julai mwaka huu. Rais Magufuli anagombea kwa mara ya pili baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

error: Content is protected !!