October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Membe, Maalim Seif kuteuliwa na ACT-Wazalendo kugombea urais Tanzania, Z’bar?

Bernard Membe (kulia) akiwa na Maalim Seif Sharrif Hamad

Spread the love

CHAMA cha siasa cha upinzani nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo, kinafanya mkutano mkuu wa chama hicho ukiwa na ajenga mbili kuu kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wenyewe utafanyika kwa siku mbili tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Mkutatano huo unafanyika leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa chama hicho akizungumza amesema, kati ya wajumbe 562 wa mkutano mkuu huo, wajumbe waliokwisha kujorodhesha na wapo ukumbini ni 428 sawa na asilimia 76.15 idadi ambayo inakidhi kuendelea.

“Katika mkutano huu, tutafanya uteuzi wa wagombea ngazi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais wa Zanzibar,” amesema Shaibu.

Shaibu amesema, mkutano huo pia, utapokea taarifa ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa upande wa Zanzibar na Tanzania.

Katika nafasi ya wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyejitokeza kuchukua na kurejesha fomu ni mmoja, Bernard Membe ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo.

Upande wa mgombea urais wa Zanzibar, aliyechukua na kurejesha fomu ni mmoja, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Viongozi waliohudhuria; Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatuma Karume, Msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali.

error: Content is protected !!