Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sadaka misa ya Mkapa kukarabati nyumba ya mapadri Lupaso
Habari Mchanganyiko

Sadaka misa ya Mkapa kukarabati nyumba ya mapadri Lupaso

Marehemu Benjamin Mkapa
Spread the love

YUDA Rua’ichi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam ameagiza, sadaka itakayopatikana kwenye shughuli ya kumuaga Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya tatu zitumike kukarabati nyumba ya mapadri ya Lupaso, Mtwara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetangazwa leo tarehe 26 Julai 2020, kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam ambapo sala na shughuli ya kuaga mwili wa Mzee Mkapa aliyefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020, zikiendelea.

“Mzee Mkapa alikuwa na nia ya kukarabati nyumba ya mapadri ya parokia ya Lupaso, ukarabati huo unakadiriwa kutumia si chini ya Sh. 20 milioni. Hiyo nyumba tangu ilipojengwa na wale wamisionari wa kwanza, haijafanyiwa ukarabati.”

“Mhashama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Rua’ichi kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Tanzania, ameagiza sadaka hii ya leo itakuwa ni kwa ajili ya kumuenzi mzee wetu kwa ukarabati wa nyumba hiyo,” imeeleza taarifa hiyo.

Misa ya kumuaga mwili wa Rais Benjamin Mkapa

Shuhuli ya kuaga mwili wa Mzee Mkapa itafanywa kwa siku tatu kuanzia leo hadi Jumanne tarehe 28 Julai 2020 na kisha, atapelekwa kuzikwa kijijini kwake Lupaso, Mtwara Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!