Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Ngalalekumtwa atoa somo kifo cha Mkapa
Habari Mchanganyiko

Askofu Ngalalekumtwa atoa somo kifo cha Mkapa

Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa
Spread the love

ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa, amewataka Watanzania kutafakari matendo yao kama yanampendeza Mungu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kiongozi huyo wa kiroho, ametoa wito huo leo Jumapili tarehe 26 Julai 2020 wakati wa mahubiri yake kwenye misa ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa, katika Viwanja vya Uhuru, Dar es Salaam.

Viongozi na mamia ya wananchi wanaendelea kumiminika katika viwanja vya Uhuru kwa ajili ya kushiriki ibada hiyo na kuaga mwili wa Mkapa aliyefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na viongozi wengine waliohudhuria katika misa hiyo.

Katika mahubiri yake, Askofu Ngalalekumtwa amewataka Watanzania kujiuliza kama maisha yao hapa duniani yanampendeza Mungu na ni baraka kwa wengine.

“Na tujiulize je, hija yangu ya hapa duniani ni baraka kwa ajili ya wenzangu? Tunajiuliza maana tuliambiwa omba unachokitaka na mimi nikupe hicho nilichokiomba, je ni kitu sahihi kwa vigezo vyote?” asemaAskofu Ngalalekumtwa.

Askofu Ngalalekumtwa amesema pasipo uwepo wa Mungu hakuna jambo litakalokuwa thabiti na kuwataka Watanzania kuomba huruma ya Mungu ili waweze kutumia vyema nafasi ya kuishi katika dunia hii.

Misa ya kumuaga mwili wa Rais Benjamin Mkapa

“Sala kuu ya Jumapili ya leo tulioisali, inaungama kwamba pasipo Mungu hakuna lililothabiti, pasipo Mungu hakuna lililotakatifu. Hivyo, sala inaendelea kuomba huruma ya Mungu ili tujaliwe tuweze kutumia vyena mambo ya dunia hali tumeambatana na ya milele,” amesema Mhasham Ngalalekumtwa.

Amesema, Watanzania wakitumia vyema mambo ya dunia katika mtazamo wa maisha baada ya kufa, itasaidia kukumbusha wanadamu kwamba wanatakiwa kuishi kwa manufaa ya wengine.

“Tukiyatumia vyema mambo ya dunia na tukiwa na mtazamo kwenye umilele hapo ndio akili, hiyo ndio hekima, huo ndio mpango kazi wenye tija kwamba ninezawaidia maisha hayo na nimeishi si manufaa yangu mimi bali kwa wenzangu,” amesema Mhasham Ngalalekumtwa.

Amewataka Watanzania kumuombea Mkapa ili Mungu airehemu roho yake, ipumzike kwa amani.

“Hivyo wapendwa, nyote tupeleke sala zetu kwa baba wa milele, maombi yetu, dua zetu maombolezo yetu yaende kwa baba wa milele kusudi mzee wetu huyu ambaye tunaimani kubwa juu ya huruma ya Mungu na upendo wake, amjalie kukaribishwa kwenye mji wa wenye haki aweze kukumbatiwa kifuani pa Ibrahim baba yetu wa imani kipenzi wa Mungu,” amesema Askofu Ngalalekumtwa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!