Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Butiku: Ukiondoka madarakani, usiwachagulie Watanzania kiongozi
Habari za Siasa

Butiku: Ukiondoka madarakani, usiwachagulie Watanzania kiongozi

Spread the love

JOSEPH Butiku, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakina tabia ya kuwachaguliwa Watanzania rais na huo ulikuwa msimamo wa Hayati Benjamin William Mkapa. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Akimzungumzia Mzee Mkapa, Rais wa awamu ya tatu aliyefariki usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020, Butiku, aliyewahi kuwa msaidizi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere amesema, miongoni mwa sifa yake Mkapa ni kuishi kutokana na mtizamo wa chama chao – CCM.

“Katika chama chetu (CCM) hatuna tabia ya rais anayeondoka madarakani kuwachaguliwa Watanzania kiongozi. Yalikuwa ni mazungumzo ya Mwalim Nyerere na Ben (Benjamin Mkapa).

“…na mimi niliwaambia Watanzania hivi, kama rais unaondoka basi acha chama chako kichague uongozi. Unaondoka na usiwachagulie kiongozi,” amesema Butiku.

Butiku ametaja sifa ya kipekee ya Mkapa kabla ya kuingia Ikulu, ni kuwa na ufanisi mkubwa wa lugha ya Kiingereza na kwamba aliwashinda hata baadhi ya Waingereza.

“Mkapa alikuwa akijua Kingereza kuliko mtu yeyote pamoja na baadhi ya Waingereza. Kwa sababu Makerere (Chuo Kikuu cha Makerere) alifanya B:A Literature owners, huwezi kufanya hiyo Makerere kama humudu kingereza na kama hukufundishwa katika mazingira ya kingereza,” amesema Butiku.

Amesema, kutokana na lugha yake kuwa nzuri, alielewana sana na Mwalimu Nyerere na ndio maana alikuwa akiandika kila alichosema Mwalimu Nyerere kwa ufasaha.

Pia, ametaja namna Mkapa alishindwa kuvumilia magazeti yaliyoonekana ‘kuyumba,’ kwa kuwa naye (Mkapa) alikuwa ni mwandishi.

“…ila alikuwa na utofauti kidogo na watu wa magazeti, alikuwa anaona kwamba wapo ambao wakati mwingine alikuwa hawana umakini unaostahili katika kazi yao,” amesema.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali. Pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!