Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Shein: Tujifunze utawala bora kwa Mkapa
Habari za Siasa

Dk. Shein: Tujifunze utawala bora kwa Mkapa

Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Shein, Rais wa Zanzibar amewataka viongozi wa sasa kujifunza utawala bora kutoka kwa Hayati Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam …. (endelea).

Amesema, Mzee Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia jana tarehe 24 Julai 2020, jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tayari ameacha funzo la utawala bora kwa viongozi wa sasa na wajao.

Dk. Shein ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Julai 2020, nyumbani kwa Mkapa, Masaki jijini Dar es Salaam, alipokwenda kuipa pole familia ya rais huyo.

Amesema, viongozi waliopo madarakani wanapaswa kujifunza kutokana na uongozi wa Rais Mkapa, aliyeongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

“Viongozi waliopo madarakani wanapaswa wajifunze kwa marehemu Mkapa, wajifunze uongozi wake. Wale viongozi wa leo tujifunze na amesadifu vizuri. Ameandika kitabu chake,” amesema Rais Shein na kuongeza:

“Tumepata msiba mkubwa kwenye taifa letu na kwa Afrika. Mkapa ni kiongozi wetu, sisi wengine ametulea. Mimi aliniteua Makamu wa Rais, nilifanya naye kazi karibu miaka minne na nusu na nimejifunza mengi,” amesema.

Dk. Sheikn amesema, Mzee Mkapa aliitumikia nchi kwa heshima na nidhamu kubwa, alisimamia misingi ya uchumi wa nchi na maendeleo yake.

Amesema, atamkumba Rais Mkapa kwa mambo mengi ikiwemo uanzishwaji wa utawala bora pamoja na kuleta mageuzi ya kiuchumi.

“Nayakumbuka mengi sana, amesaidia kuibadilisha nchi. Ameanzisha utawala bora, amebadilisha uchumi na alikua wa kwanza kuanzisha Wizara ya Utawala Bora Afrika,” Amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!