Wednesday , 6 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: Viongozi wastaafu wajifunze kwa Mkapa
Habari za Siasa

Dk. Bashiru: Viongozi wastaafu wajifunze kwa Mkapa

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM
Spread the love

CHAMA tawala nchini Tanzania Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, kitamkumbuka Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin William Mkapa jinsi alivyokijenga chama hicho na kuperusha vyema bendare ya CCM. Anaripoti Regina Mkonde,Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alipofika nyumbani kwa Mkapa, Masaki jijini Dar es Salaam kutoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Mkapa aliyeongoza Tanzania kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, amefikwa na mauti usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Dk. Bashiru amesema, Mkapa katika uongozi wake aliiimarisha CCM kutokana na utekelezaji wake uliotukuka wa Ilani ya chama hicho.

          Soma zaidi:-

Katibu huyo wa CCM amesema, Mkapa alifanya vizuri katika mapambano ya vita dhidi ya rushwa na utawala bora.

“Kiongozi anayekiwakilisha chama kama Rais akitekeleza ilani vizuri, inakuwa msingi wa kukiimarisha chama. Katika maeneo ya kupambana na umasikini, rushwa, misingi ya uchumi wa kitafa.”

“Tunamkumbuka kama mpeperusha bendera mzuri, alituacha katika hali nzuri na kipindi cha uchaguzi tulishinda vizuri,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru ameshauri Watanzania kuyaenzi mazuri aliyofanya Mkapa katika kipindi chote.

“Tumshukuru Mungu kwa kutujalia kupata kiongozi wa aina yake. Tumuoembee maisha na mapumziko huko mbeleni. Kilio kitakoma na machozi yatakauka lakini mchago wake uliotukuka utakumbukwa milele,” amesema Dk. Bashiru.

“Ningeomba tuenzi kwa vitendo yale aliyotuachia. Amejenga taifa lake, alijenga uchumi wa taifa letu, amesuluhisha migogoro katika mataifa mbalimbali na amelitangaza taifa ulimwengu katika diplomasia,” amesema.

Dk. Bashiru amesema, kifo cha Mkapa ni pigo kwa Taifa na kwa Watanzania kwa ujumla.

Katibu huyo wa CCM amesema, ili Tanzania iuenzi mchango wake, inatakiwa iendeleze mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake.

“Sisi kazi yetu ni kuenzi aliyosimamia upendo, msimamo katika utu. Haya yanatufanya sisi tuendelee kuamini, kuondoka kwake ni pengo sababu tulimhitaji lakini kupitia matendo yake tutaendelea kumuenzi,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru amesema, Mkapa alikuwa si kiongozi wa Tanzania peke yake, bali alikuwa kiongozi wa Kimataifa.

“Alikuwa msuluhishi wa migogoro ya kimataifa, Kenya na Burundi aliwasuluhisha, alikua kiongozi wa taifa na kitaifa. Kila kiongozi mstaafu ajue ana mchango katika taifa pindi anapostaafu,” amesema Dk. Bashiru

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!