Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Kenyatta, Odinga waomboleza kifo cha Mkapa
Habari Mchanganyiko

Rais Kenyatta, Odinga waomboleza kifo cha Mkapa

Spread the love

UHURU Kenyatta, Rais wa Kenya ameomboleza kifo cha Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu wa Tanzania, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa tarehe 24 Julai 2020, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa za kifo cha Rais mstaafu Mkapa zimetangazwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli, huku kiongozi huyo wa Tanzania ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia msiba huo mzito uliowakuta Watanzania.

Mkapa aliiongoza Tanzania katika vipindi viwili mfululizo, kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alikuwa Rais wa kwanza tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992 na uchaguzi wake kufanyika mwaka 1995.

         Soma zaidi:-

Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya, ametuma salamu za rambirambi kwa Rais Magufuli, familia ya marehemu Rais Mkapa pamoja na Watanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Julai 2020, na Ikulu ya Kenya kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Kenyatta amemwelezea Mkapa kwamba alijituma bila kuchoka kuleta maendeleo ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

“Katika ujumbe wake wa faraja, Rais Kenyatta ameomboleza kifo cha kiongozi wa Tanzania, aliyekuwa kiongozi bora Afrika Mashariki aliyefanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya usuluhishi, amani na maendeleo,” inaeleza taarifa ya Ikulu ya Kenya.

Raila Odinga, Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini Kenya, Orange Democratic Movement (ODM), ameomboleza kifo cha nguli huyo wa siasa, akisema Mkapa alikuwa rafiki mkubwa wa wananchi wa Kenya.

Odinga amesema, Wakenya watamkumbuka Mkapa, kutokana na juhudi zake za kuleta amani nchini Kenya akishirikiana na Dk. Koffi Annan na Graca Machel, baada ya taifa hilo kukumbwa na machafuko ya kisiasa, yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa 2008.

“Mkapa aliamini katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika imepoteza mtu mkubwa, maombi yangu yako familia, Rais Magufuli na watu wa Tanzania,” ameandika Odinga katika ukurasa wake wa Twitter.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

error: Content is protected !!