Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Urais Z’bar: CCM yapendekeza majina 5
Habari za Siasa

Urais Z’bar: CCM yapendekeza majina 5

Prof. Makame Mbarawa (kulia) mmoja ya watia nia ya Urais Zanzibar wakati anarudisha fomu za kuwania urais
Spread the love

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, imependekeza majina matano kati ya 31 ya wanachama wa chama hicho waliojitokeza kugombea urais visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wagombea hao 31, walichukua na kurejesha fomu kati ya tarehe 15 hadi 30 Julai 2020 za kuwania kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 hatogombea kwani amemaliza muda wake Kikatiba.

Miongoni mwa wagombea hao 31, kuna watoto wa marais wastaafu, viongozi waliopo serikalini na wastaafu.

Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM, imekutana leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020 chini ya Makamu mwenyekiti l
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi, akizungumza na waandishi wa habari amesema, kamati hiyo ni sehemu muhimu ya maandalizi na uchujaji wa majina ya wagombea watano wanaotakiwa kuwasilishwa katika Kamati Kuu.

Amesema, majina hayo yatawasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa tena na kumtafuta mgombea bora mwenye sifa 12 zikiwemo hekima, kuaminika, kuthamini muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Hussein Mwinyi (kulia) mmoja ya watia nia ya Urais Zanzibar wakati anarudisha fomu za kuwania urais

Dk. Mabodi amesema, baada ya Kamati kuu kujadili kwa kina majina hayo matano, itapendekeza majina matatu na kuyapeleka Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambayo itachagua na kupatikana jina moja.

          Soma zaidi:-

Amesema, baada ya hatua hiyo, mgombea huyo atapelekwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kwa ajili ya kudhibitishwa na kupata baraka za Wajumbe wote wa kamati kuu.

Ametumia fursa hiyo, viongozi kwa ukomavu wao wa kisiasa kwa kufuata Katiba,miongozo na Kanuni za CCM kwa kutobeba wagombea mifukoni jambo ambalo lingeleta shida ikiwemo mpasuko.

Maudline Cyrus Castico, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wanawake, Wazee na Watoto Zanzibar akipokea fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya CCM

Amesema, kikao hicho kimesisitiza usiri kwa majina hayo matano ya wagombea kwani ndani ya chama ikibainika kuna aliyekiuka taratibu atachukuliwa hatua za kinihamu ikiwemo kumwondoa.

“Lazima tuenzi siri za vikao, ni muhimu watu wote kuheshimu maamuzi ya vikao na kufuata utaratibu uliowekwa ndani ya Chama cha Mapinduzi,” amesema Dk.Mabodi.

Majina 31 ya waliojitokeza ni;

1. Mbwana Bakari Juma
2. Balozi Ali Abeid Karume
3. Mbwana Yahya Mwinyi :
4. Omar Sheha Mussa
5. Dk. Hussein Ali Mwinyi
6. Shamsi Vuai Nahodha
7. Mohammed Jaffar Jumanne
8. Mohammed Hijja Mohammed
9. Issa Suleiman Nassor
10. Profesa Makame Mabarawa
11. Mwatum Mussa Sultan
12. Haji Rashid Pandu
13. Abdulhalim Mohammed Ali
14. Jecha Salum Jecha
15. Dk. Khalid Salum Mohammed
16. Rashid Ali Juma
17. Khamis Mussa Omar
18. Mmanga Mjengo Mjawiri
19. Hamad Yussuf Masauni
20. Mohammed Aboud Mohammed
21. Bakari Rashid Bakari
22. Ayoub Mohammed Mahmoud
23. Hashim Salum Hashim
24. Hasna Atai Masound
25. Fatma Kombo Masound
26. Iddi Hamadi Iddi
27. Pereira Ame Silima
28. Shaame Simai Mcha
29. Mussa Aboud Jumbe
30. Mgeni Hassan Juma
31. Maudline Cyrus Castico

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

error: Content is protected !!