Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa akerwa wahamiaji haramu Katavi kukithiri, RC…
Habari Mchanganyiko

Majaliwa akerwa wahamiaji haramu Katavi kukithiri, RC…

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa Katavi
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka watu wanaoishi kwenye makazi ya Mishamo na Katumba wawe waadilifu na wasitumike kama madalali wa kuingiza wahamiaji haramu nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi … (endelea).     

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mkoa wa Katavi umekithiri kwa kuwa na wahamiaji haramu wengi, hivyo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi (RC), Juma Homera ashughulikie tatizo hilo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020 alipozindua jengo la ofisi na biashara la Mpanda Plaza lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Mpanda kwa gharama ya Sh. 2.8 bilioni.

“Katavi imetulia lakini haijatengamaa kwa sababu ni kati ya mikoa yenye idadi kubwa ya wahamiaji haramu nchini ambao njia yao wanayotumia kuingilia Katavi ni makazi ya Katumba na Mishamo,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua zao la pamba mara baada ya kuzindua soko la zao hilo Katavi

Waziri mkuu amesema, Tanzania haijazuia watu wa Mataifa mengine kuingia nchini ila inawataka wafuate taratibu zilizowekwa na si kuingia kwa kutumia njia za panya.

Amesema anamajina ya watu zaidi 2,000 walioingia Tanzania kwa njia za panya na wamejiingiza katika maeneo mbalimbali,  amewataka warudi kwao na wafuate taratibu kabla ya kuja tena nchini.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa Mpanda Plaza, Majaliwa ameliponeza Shirila la Nyumba la Taifa kwa uwekezaji huo ambao utaliwezesha shirika hilo kujiongezea tija.

Kadhalika, waziri mkuu amelielekeza shirika hilo kwenda kujenga majengo ya makazi katika wilaya mpya ili kuwawezesha watumishi na wananchi kuishi kwenye makazi bora.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani amesema, uzinduzi wa jengo hilo la ghorofa tano ni muendelezo wa miradi iliyowekezwa na NHC kwa gharama ya Sh. 7.2 bilioni mkoani Katavi.

Jengo la Mpanda Plaza lililopo Mpanda, mkoa wa Katavi

Dk. Banyani amesema miradi mingine iliyowekezwa na NHC mkoani Katani ni pamoja na ujenzi wa nyumba 70 eneo la Ilembo, nyumba 24 katika mji wa Inyonga, Mlele.

“Tumejenga nyumba tano za Wakuu wa Idara halmashauri ya Wilaya ya Mlele, nyumba 24 za walimu katika shule ya msingi Kakuni, nyumba sita shule ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe,” amesema.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Homera alisema miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinaukabili mkoa huo ni majangili ambapo waliendesha operesheni na kufanikiwa kikamata silaha 100.

Alisema kwa sasa wananchi wanaendelea kufanya kazi na kwamba ukusanyaji wa mapato umeongeza kutoka asilimia 76 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 97 mwaka huu.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa mbali na kuboresha ukusanyaji wa mapato, pia wameimarisha upatikanaji huduma za afya hususani kwa mama na mtoto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!