Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika: Nguvu ya umma itaamua uchaguzi mkuu 2020
Habari za Siasa

Mnyika: Nguvu ya umma itaamua uchaguzi mkuu 2020

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
Spread the love

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema kimesema, kitatumia nguvu ya umma, kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020 na John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema, wakati anafungua mafunzo ya wagombea urais, ubunge na udiwani  katika Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam.

Mnyika amesema, Chadema imeamua kutumia nguvu ya umma, baada ya jitihada za upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi kugonga mwamba.

Katibu huyo wa Chadema amesema, Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, utakuwa ni wa nguvu ya umma.

“Watawala wamesema watatumia nguvu ya dola kubaki madarakani, ndio maana wamekataa agenda ya tume huru ili uchaguzi usifanyike huru.”

          Soma zaidi:-

“Sababu wamekataa tume huru na njia za kawaida na wamejitangaza wazi kubaki madarakani,  sisi tunatangaza tutatumia nguvu ya umma kuingia madarakani,” amesema Mnyika.

Amesema, katika chaguzi zilizopita Chadema kilipata ushindi katika majimbo kadhaa, kutokana na nguvu ya umma, baada ya wagombea wake walioshinda kutotangazwa na wakurugenzi wa uchaguzi.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

Mnyika amesema, katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na wa 2015, kuna baadhi ya maeneo wakurugenzi wa uchaguzi waligoma kutangaza wagombea wa Chadema walioshinda ubunge na udiwani, lakini wananchi walisimama imara kulinda kura zao.

Katika hatua nyingine, Mnyika amesema Chadema kitazindua rasmi ilani yake ya uchaguzi, mwishoni mwa mwezi Julai 2020, katila Mkutano Mkuu ambao pia utampitisha mgombea urais.

“Mwezi Julai 2020 katika mkutano mkuu, tutazindua ilani ya uchaguzi, itaeleza kwa kina nini ambacho Chadema ikiingia madarakani itawafanyia watanzania,” amesema Mnyika.

Hivi sasa Chadema iko katika mchakato wa kupata wagombea, ambapo zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu limeanza leo na linahitaji kukamilika tarehe 10 Julai 2020 kwa wagombea ubunge na udiwani.

Huku uchukuaji na urejeshaji fomu za kugombea urais wa Tanzania litafungwa tarehe 19 Julai mwaka huu.

Endelea kufuatilia MwanaHalisi Online na MwanaHalisi TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!