Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Mwongozo uvaaji barakoa wanafunzi Tanzania watolewa
Afya

Mwongozo uvaaji barakoa wanafunzi Tanzania watolewa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imetoa mwongozo wa namna wanafunzi na walimu wa shule za msingi na sekondari, watakavyokabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mwongozo huo umetolewa jana Jumapili tarehe 28 Juni 2020 na Gerard Chami, Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano ya Serikali Idara ya Afya.

Muongozo huo umetolewa  baada ya agizo la kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari, leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020, lililotolewa na Rais John Magufuli.

Serikali ya Tanzania tarehe 17 Machi 2020, ilitangaza kufunga shule hizo, ili kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Baada ya taifa hilo kupata mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 tarehe 16 Machi 2020 jijini Arusha.

Taarifa hiyo inaeleza, pamoja na kutolewa kwa elimu kuhusiana na mwongozo huu, tunapenda kufafanua zaidi suala la matumizi ya barakoa kwa wanafunzi ili kueleweka vizuri kwa wanafunzi, walimu na wananchi.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, wanafunzi wenye matatizo ya kiafya yanayoweza kuathiri mfumo wa upumuaji, wavae barakoa, huku waalimu na viongozi wa shule, wakiagizwa kuwafuatilia kwa ukaribu wanafunzi hao.

“Watoto walio chini ya umri wa miaka nane, wanafunzi wote hata kama ana zaidi ya miaka nane wenye matatizo ya kiafya kama magonjwa ya mfumo wa upumuaji mfano pumu, matatizo ya moyo, selimundu, wenye kisukari, shinikizo la damu, unene mkubwa na wenye matatizo ya figo,” unaeleza muongozo huo.

“Na wale ambao historia yao katika uongozi wa shule inaonyesha wana matatizo ya kiafya yanayoweza kuathiri upumuaji. Wanafunzi hao wavae barakoa lakini wafuatiliwe kwa uangalizi wa karibu.”

Aidha, muongozo huo umewaagiza walimu wa madarasa na walimu wakuu, kuwa karibu na wanafunzi wao, pamoja na kutoa taarifa mapema, pindi mwanafunzi anapopata shida yoyote ya kupumua.

“Walimu wa madarasa na walimu wakuu wanaelekezwa kuwa karibu na wanafunzi katika kufuata maelekezo ya mwongozo huu, na kutoa taarifa mapema pale ambapo mwanafunzi anapopata shida yoyote kama kupumua, kuishiwa nguvu na kukohoa,” unaeleza muongozo huo.

Pia, wanafunzi wanatakiwa kuvaa barakoa wakiwa katika mazingira yenye msongamano.

Aidha, muongozo huo unaelekeza wanafunzi wenye umri zaidi ya miaka nane, ambao hawana matatizo ya kiafya, wasivae barakoa.

“Mwongozo unaelekeza wanafunzi watumie barakoa katika mazingira ya msongamano, aidha, wanafunzi hawapaswi kuvaa barakoa wakati wa michezo au wakiwa wanafanya mazoezi mengine ikiwemo kukimbia mchakamchaka,” unaeleza mwongozo huo.

Hata hivyo, Serikali imetoa wito kwa wadau kutoa maoni yao kuhusu utekelezaji wa mwongozo huo, ili kuufanyia marekebisho.

“Pamoja na uzoefu wa kisayansi tunaoupata kuhusiana na ugonjwa huu, na kwa kuzingatia mazingira yetu, wizara itaendelea kufuatilia kwa karibu  sana utekelezaji wa mwongozo kuhusu matumizi sahihi ya barakoa kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na changamoto zinazojitokeza,” unaeleza mwongozo huo

“Aidha, wadau, wazazi na walezi wanakaribishwa kutoa maoni yao kuhusu utekelezaji wa mwongozo huo iwapo italazimika kuboreshwa ili kuwalinda wananfunzi.”

1 Comment

  • Mi naona serikali ingetoa elekezi kwa shule za bordings watoto wapewe maji ya moto wanywe kila siku jioni na wasukutue midomo yao na maji ya uvuguvugu ya chumvi ikabla ya kwenda kulala nasaidia sana .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!