May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwanamke wa tano achukua fomu Z’bar kugombea urais  

Maudline Cyrus Castico, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wanawake, Wazee na Watoto Zanzibar akipokea fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya CCM

Spread the love

MAUDLINE Cyrus Castico, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wanawake, Wazee na Watoto Zanzibar, amekuwa mwanachama wa 32 kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Castico amekabidhiwa fomu hiyo na Cassian Gallo’s, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC idara ya Oganaizesheni Zanzibar, katika Ofisi Kuu ya CCM iliyoko Kisiwandui.

Waziri huyo mwenye dhamana ya amsuala ya uwezeshaji wanawake na watoto Zanzibar, amekuwa mwanamke wa tano kujitosa katika kinyang’anyiro hicho, tangu zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu ndani ya CCM, kufunguliwa tarehe 15 Juni 2020.

Wanawake wengine waliochukua fomu hiyo ni,  Mgeni Hassan Juma, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mwantum Mussa Sultan, Hasna Atai Masoud na Fatma Kombo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Castico amesema amechukua fomu ili kuwapa hamasa wanawake kugombea katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

“Niwahakikishieni kwamba nia yangu ni safi na nimekuja kwa makusudi kwa ajili ya kutaka kuungana na wenzaagu walioomba. Lakini lingine lililonisukuma ni kuona kwamba, kati ya wagombea 32, wanawake tuko watano,” amesema Castico na kuongeza:

“Sasa hivi tunaenda kwenye uchaguzi, kwenye nafasi za ubunge na nafasi mbalimbali kwenye maeneo mengi, nikaona tusipoonesha mfano kama viongozi haitakuwa vizuri. Nikaona ni vyema niweze kuwa chagiza wenzangu, wawe na moyo wa kugombea kwenye nafasi zilizopo, popote walipo.”

Castico amewataka wanawake kujiamini, na kujitosa kugombea kwenye nafasi mbalimbali, ikiwemo urais, ubunge, udiwani na uwakilishi, kwa kuwa wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

 

Hasna Atai Masoud

“Wanawake waende kwa kujiamini kwa kutetea haki yao, kwa kuwa wana mchango mkubwa katika taifa, na wana mambo mengi na wanaimani sana,” amesema Castico.

Hadi sasa kw aupande wa urais wa Zanzibar wanawake waliojitokeza kuchukua fomu ni 5, huku wanaume waliojitokeza ni 27.

Wagombea 31 wa awali waliojitokeza ni;-

 1. Mbwana Bakari Juma
  2. Balozi Ali Abeid Karume
  3. Mbwana Yahya Mwinyi :
  4. Omar Sheha Mussa
  5. Dk. Hussein Ali Mwinyi
  6. Shamsi Vuai Nahodha
  7. Mohammed Jaffar Jumanne
  8. Mohammed Hijja Mohammed
  9. Issa Suleiman Nassor
  10. Profesa Makame Mnyaa Mabarawa
  11. Mwatum Mussa Sultan
  12. Haji Rashid Pandu
  13. Abdulhalim Mohammed Ali
  14. Jecha Salum Jecha
  15. Dk. Khalid Salum Mohammed
  16. Rashid Ali Juma
  17. Khamis Mussa Omar
  18. Mmanga Mjengo Mjawiri
  19. Hamad Yussuf Masauni
  20. Mohammed Aboud Mohammed
  21. Bakari Rashid Bakari
  22. Hussein Ibrahim Makungu
  23. Ayoub Mohammed Mahmoud
  24. Hashim Salum Hashim
  25. Hasna Atai Masound
  26. Fatma Kombo Masound
  27. Iddi Hamadi Iddi
  28. Pereira Ame Silima
  29. Shaame Simai Mcha
  30. Mussa Aboud Jumbe
  31. Mgeni Hasaan Juma
error: Content is protected !!