Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nyalandu: Nitafanya mabadiliko Tanzania, Chadema
Habari za Siasa

Nyalandu: Nitafanya mabadiliko Tanzania, Chadema

Lazaro Nyalandu, mtia nia wa Urais kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

LAZARO Nyalandu, mtia nia wa urais wa Tanzania ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, akipewa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atafanya mabadiliko ndani ya nchi na ndani ya chama chake. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Nyalandu ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Kati ameyasema hayo leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 katika mahojiano kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.

Nyalandu ni miongoni mwa watia nia 11 wa Chadema katika mbio za urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Nyalandu ambaye ni waziri wa zamani wa malisili na utalii enzi za utawala wa awamu ya nne ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ameweka wazi vipaumbe vyake 26 endapo chama chake na Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza atavifanya ndani ya siku 100 za mwanzo.

Katika mahojiano hayo, Nyalandu amesema, akishika madaraka ataanza kufanya mabadiliko ndani ya Chadema chama ambacho kwa sasa kinaongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe.

Amesema, Mbowe amekivusha chama hicho kwenye nyakati ngumu bila kupoteza mvuto.

Nyalandu amesema, chama hiki kinachangamoto ya ndani ambayo ni Itifaki ambayo inayohitajika kurekebishwa mfumo huo ndani ya chama.

“Namna gani wakati gani uongee nini, wakati gani usiongee, wakati gani usikilize, wakati gani upambane kwelikweli kila kitu kina muda wake,” amesema Nyalandu ambaye amesema hata asipopitishwa kugombea hatokuwa na kinyongo na watamuunga aliyepewa fursa hiyo

Kuhusu mabadiliko ya nchi, Nyalandu amesema, hana mpango wa kubomoa kile kilichojengwa na watangulizi wake, “tunampango wa kujenga juu ya misingi iliyowekwa, kuna mambo tutayaboresha, kuna mambo tutayabadilisha ikibidi na kuna mambo mapya tutayaleta.”

     Soma zaidi:-

Amesema, kipekee ataboresha mtaji kwenye Benki ya Wanawake kupitia benki za kimataifa ili wanawake wapate fursa ya kupata mikopo na amana za fedha ili kuongeza fursa za kibiashara.

“Sisi tukipata fursa ya kuchukua dola, tutaboresha benki ya wanawake, tutahakikisha msichana anapata fursa sawasawa na mvulana kwenye elimu na ajira,” amesema Nyalandu

Amesema upande wa mirathi, kutakuwepo na sheria itakayomlinda mjane kwenye mirathi, pia kwenye ajira wanaweka watalipwa sawa na wanaume.

Kuhusu elimu, amesema Serikali yake itatunga sheria ya ulazima wa kila shule ya kata kuwepo kwa matumizi ya kompyuta na kuunganishwa na mkongo wa taifa ili kuruhusu wanafunzi na walimu kunufaika na Tehema.

Dk. Maryrose Majinge, kada wa Chadema aliyetangaza nia ya kuwania Urais kupitia chama hicho

“Tutahakikisha kiengereza kinaanza kufundishwa darasa la kwanza ili wanafunzi wa shule za msingi wasitofautiane na wanafunzi wa shule binafsi”

“Nimefikiria wakati nakuja tunamfanyaje mwanafunzi, kunavitu vya kishamba kuchapa, kupiga viboko tutafuta adhabu ya viboko kwa sababu adhabu ya viboko haisaidii,” amesema.

Nyalandu amesema baada ya kutangaza kujiuzulu ubunge wa Singida Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 30 Oktoba 2017, aliamua kukaa kimya ili kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na uongozi pindi alipojiunga na Chadema.

“Nilipumzika nilipojiuzulu nyazifa zangu nyengine kwenye, maisha tunahitaji kutulia, kuangalia wanavyofanya kazi, jifunze kwa  mazuri wanayofanya, angalia yale ambayo mapungufu.”

“Angalia fursa hiyo inakuja kwamba kuna watu wanafanya mazuri lakini yanaweza, kufanyika makubwa zaidi na katika harakati hizi za kuleta mabadiliko ambayo wote tunayataka, nikajifunza mengi wakati wa utulivu wangu,” amesema

Watia nia wengine 10 wa Urais ndani ya Chadema ni;

  1. Isaya Mwita
  2. Lissu Tundu A.M
  3. Dk. Majinge, Mayrose Kavura
  4. Manyama Leonard Toja
  5. Mbowe, Freeman Aikael
  6. Mchungaji Msigwa, Peter Simon
  7. Wakili.  Mwanalyela, Gasper Nicodemus
  8. Nalo, Opiyo G.O.M
  9. Wakili Neo, Simba Richmund
  10. Shaban, Msafiri

Waliotia nia kugombea urais Zanzibar

  1. Hashim Juma Issa
  2. Mohammed Ayoub Haji
  3. Said Issa Mohammed

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!