Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Urais Z’bar: Mbwana afungua pazia CCM
Habari za Siasa

Urais Z’bar: Mbwana afungua pazia CCM

Mbwana Bakari Juma, kada wa CCM
Spread the love

MBWANA Bakari Juma amefungua pazia la uchukuaji wa fomu za kuomba kupitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo umeanza leo Jumatatu tarehe 15 hadi 30 Juni, 2020 kwa wanaotaka kugombea urais wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujitokeza.

Juma amekuwa wa kwanza kufika Ofisi Kuu CCM zilizopo Unguja, Zanzibar. Mara baada ya kukabidhiwa fomu, akasema amejitahimini na kuona anafaa kuwa Rais wa visiwa hivyo.

Amesema, licha ya kuwa Urais ni kazi ngumu lakini hilo litawezekana kwa kudra za Mwenzi Mungu kwani ili atimize majukumu yake lazima we mnyenyekevu, mwadilifu mwenye moyo wa kujitoplea.

Juma amesema, endapo chama hicho kitampitisha na kuwa mgombea urais na Wazanzibar kumpigia kura za kutosha na kuwa Rais, atahakikisha anaweka mbele maslahi ya wananchi.

Amesema, Rais Ali Mohamed Shein, amefanya kazi kubwa nay eye akipitishwa ataendeleza yale aliyoyafanya.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!