Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kilichozungumzwa kati ya Magufuli na Rais mteule wa Burundi
Habari za Siasa

Kilichozungumzwa kati ya Magufuli na Rais mteule wa Burundi

Evariste Ndayishimiye, Rais wa Burundi
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amezungumza kwa njia ya simu na Rais Mteule wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye na kumpongeza kwa uamuzi wa Mahakama ya Katiba nchini Burundi iliyoagiza Rais Mteule aapishwe haraka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemtakia heri, Rais Mteule Ndayishimiye kuelekea kuapishwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Burundi kutakakofanyika hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi tarehe 13 Juni 2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli amemhakikishia Rais Mteule Ndayishimiye kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa karibu na Burundi kwa kuwa nchi hizo ni majirani, marafiki na ndugu wa kihistoria.

Rais John Magufuli

Rais Magufuli amerudia kumpa pole kwa msiba wa kuondokewa na Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza aliyefariki dunia tarehe 09 Juni, 2020 na amemueleza kuwa yeye na Watanzania wote wanaungana na Warundi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Amemuomba kufikisha salamu zake za rambirambi kwa Warundi wote na kuwasihi waendelee kuwa watulivu na wastahimilivu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!