Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wananchi walivyozungumzia miaka mitano Ubunge wa Kubenea
Habari za Siasa

Wananchi walivyozungumzia miaka mitano Ubunge wa Kubenea

Wadau wa Jimbo la Ubungo
Spread the love

WADAU katika Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, wamezungumzia miaka mitano ya utumishi wa Saed Kubenea, mbunge wa jimbo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam….(endelea). 

Wadau hao wametoa ya moyoni kuhusu utendaji wa Kubenea katika mkutano wa mbunge huyo na wadau wa jimbo hilo, uliofanyika leo Jumamosi tarehe 13 Juni 2020 Sinza jijini Dar es Salaam

Katika nyakati tofauti, wadau hao wamesema, katika utendaji wake Kubenea, alifanya mambo mengi kwa ajili ya kuondoa changamoto za wananchi wa jimbo hilo.

Charles Paul, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema, kwa kazi aliyoifanya Kubenea, kama atagombea tena atashinda jimbo hilo.

“Kwa kazi aliyoifanya, naamini kama goma linapigwa 2020 jimbo (Ubungo) tunaondoka nalo,” amesema Paul.

Paul amesema, Kubenea alitatua changamoto mbalimbali za wananchi wa jimbo lake, ikiwemo changamoto ya uhaba wa maji kwa  kuchimba visima kadhaa, pamoja na kutumia sehemu ya fedha za mfuko wa bunge, kuwainua wananchi wake kiuchumi.

“Amechimba kisima soko la Mabibo, fedha ya mfuko wa ubungo kila eneo anapeleka  bila kubagua mtu yoyote. Hilo sio suala la kuzungumza sana kikubwa tunakwenda 2020 tusimame kwa pamoja kuhakikisha ubungo inabaki Chadema na si chama kingine chochote,” amesema.

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo

Raphael Mlay, aliyekuwa Mwenyekiti Mtaa wa Baruti- Kimara kupitia Chadema, amesema, mambo aliyoyafanya Kubenea yanatosha kumrudisha tena.

Mayunga Kadwisha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabibo kupitia Chadema, amesema, Kubenea aliusaidia mtaa wake hususan katika Soko la Mabibo, kwa kulikarabati soko hilo.

“Soko la Mabibo amekarabati Kubenea tumrudishe tupuuze wanaosema hakuna kitu amefanya,” amesema Kaswisha.

Baadhi ya wananchi wa jimbo la Ubungo hawakuwa nyuma katika suala hilo, ambapo wamesema watamkumbuka Kubenea kutokana na moyo wake wa kuwainua kiuchumi, kwa kuwapa mikopo isiyo na riba kupitia fedha za mfuko wa jimbo hilo.

Ramadhani Kijiwe, Mkazi wa Mabibo, amesema, “Tulipata mikopo isiyokuwa ya riba, tumejikwamua kuimarisha kwa mikopo iliyotoka mfuko wa jimbo, tumejikwamua kiuchumi.”

Joseph william Kessy, Mkazi wa Mabibo amesema, Kubenea aliwadhamini yeye na wananchi wenzake kadhaa, kupata mkopo benki.

“Alitupatia pikipiki sisi ni watu ulitupa vifaa vyote vya ofisi yetu, ulitudhamini benki tukapata mkopo mkubwa, ulionesha ubinadamu wako, ulikuwa na mkono wa kutoa hukua na mkono wa birika kama utachukua fomu tutakuwa pamoja,” amesema Kessy.

Ashura Kalovya, Mkazi wa Ubungo, amesema Kubenea amewasaidia kwa mengi, na kuahidi kumpigia kura tena kama atataka kugombea jimbo hilo.

“Umetusaidia kwa mengi Mungu akusaidie, umefanya mambo mengi makubwa, nakuombea chukua fomu tuko nyuma yako tutakupigia kura tena,” amesema Kalovya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!