Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yakwamisha kesi ya Idriss
Habari Mchanganyiko

Serikali yakwamisha kesi ya Idriss

Idriss Sultani wa kwanza kushoto akiwa na wakili wake Benedict Ishabakaki
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi inayomkabili Idriss Sultani, Msanii wa Vichekesho na mwenzake Innocent Maiga baada ya upande wa serikali kushindwa kukamilisha kuandaa hoja za awali. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Tarehe 27 Mei 2020 kesi hiyo iliahirishwa hadi leo tarehe 9 Juni 2020 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali, lakini upande wa serikali umeeleza mahakama, haujamaliza kuandaa hoja za awali na kuahirishwa hadi tarehe 9 Julai 2020 kwa ajili ya kusoma hoja hizo.

Upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili Msanii wa Vichekesho, Idris Sultan na mwenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa haujakamilisha maelezo ya awali na hivyo wanaomba kupangiwa tarehe nyingine.

Mbali ya Idris Sultan, mshitakiwa mwingine ni Innocent Maiga ambapo upelelezi wa kesi yao umekamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu amehairisha kesi hiyo hadi Julai 9, 2020 huku dhamana ya washitakiwa hao zikiendelea.

Idris Sultan anakabiliwa na kosa la Kushindwa kufanya usajili wa simu kadi iliyokuwa inamilikiwa na mtu mwingine

 

Inadaiwa ametenda kosa hilo kati ya Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020 maeneo ya Mbezi Beach Kinondoni ambapo alitumia kadi ya simu iliyomilikiwa na Innocent Maiga bila kuripoti kwa mtoa leseni.

Kosa jingine ni kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya kadi ya simu ambapo linamkabili Innocent Maiga ambaye anadaiwa amelitenda Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020 Mbezi Beach Kinondoni ambapo kinyume na sheria alishindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya namba ya simu kama inatumiwa na Idris Sultan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!