Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Vyuo vikuu, michezo, ‘Form six’ kufunguliwa Juni 1
AfyaHabari za SiasaMichezoTangulizi

Vyuo vikuu, michezo, ‘Form six’ kufunguliwa Juni 1

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli ametangaza kufunguliwa kwa vyuo vyote nchini, michezo ya aina yote pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita kuanzia tarehe 1 Juni, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamisi tarehe 21 Mei, 2020 mara baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi sita aliowateua hivi karibuni Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Kasi ya maambukizi imeshuka sana, kutokana na hii hali inakwenda vizuri, tumeamua kama serikali, vyuo vyote vifunguliwe tarehe 1 Juni 2020,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kujipanga katika kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri kwa wanafunzi hao kuendelea na masomo.

https://youtu.be/5L_gBPViKxo

“Wizara ya elimu ipange mikakati, niwaombe na bodi ambayo inahusika na mikopo kwa wanafunzi, kuna siku tisa zijiandae ili vyuo vikifunguliwa pasije kuwa na kero nyingine,” amesema Rais Magufuli.

Tarehe 18 Machi 2020, Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu, aliagiza vyuo hivyo vifungwe kuepusha mikusanyiko, ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19).

Wanafunzi wa kitado cha sita wakifanya mtihani

Katika hotuba yake fupi, Rais Magufuli amesema, wanafunzi wa vyuo vikuu ni tofauti na wale wa shule za sekondari na msingi hivyo wameona waanza na vyuo kasha hali itakapokuwa nzuri watafungua na shule za sekondari na msingi.

“Kwa zile shule nyingine za sekondari na msingi zisubiri kidogo tuangalie hii ya vyuo kwa sababu ni watu wanaojitambua ni watu wazima, tujipe muda na wao baadaye tutawaoa nafasi kadri tunavyoendelea kupambana na Corona,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu wanafunzi wa kidato cha sita ambao walipaswa kufanya mitihani yao ya mwisho kuanzia tarehe 4 Mei, 2020, Rais Magufuli amesema nao warejee shuleni tarehe 1 Juni, 2020 kujiandaa na mitihani yao.

Ameagiza wizara ya elimu kuandaa mpango wa muda mfupi kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi hao kufanya mitihani yao ya mwisho ili kutokuathiri muhula wa vyuo vikuu kwa mwaka wa masomo ujayo.

Akizungumza michezo, Rais Magufuli amesema, “sina hakika kama kuna mwanamichezo aliyefariki kwa Corona Tanzania, nimeamua kuanzia tarehe 1 Juni michezo nayo ianze.”

“Ni lazima watu wafanye michezo, sasa taratibu za kuangalia na kushangilia zinaweza kupangwa lakini michezo iendelee,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

error: Content is protected !!