Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Kuna wakati Waziri Ummy alitengwa
Habari za Siasa

Rais Magufuli: Kuna wakati Waziri Ummy alitengwa

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI
Spread the love

UMMY Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewashangaa wale wote waliokuwa wakihoji alipo Rais wa Tanzania, John Magufuli katika mapambano ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Waziri Ummy amesema katika kipindi hiki cha mapambano ya corona, amejifunza mengi ikiwemo maelekezo mbalimbali aliyokuwa akiyapata kutoka kwa Rais John Magufuli ambaye alikuwa nyumbani kwake, Chato mkoani Geita.

Rais Magufuli alikuwa Chato kwa zaidi ya mwezi mmoja hadi jana Jumatano tarehe 20 Mei, 2020 aliporejea Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Waziri Ummy, akizungumza katika hafla kuapishwa kwa viongozi sita aliowateua akiwamo Dk. Godwin Mollel kuwa naibu waziri wa afya kuchukua nafasi ya Dk. Faustine Ndungulile amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake.

“Dk. Mollel umekuja kipindi hiki tunapambana na corona, kubwa ni kuwatoa hofu na Watanzania wengi walikuwa wanaumwa hofu,” amesema Waziri Ummy.

Amesema, wagonjwa wamepungua sana katika hospitali huku akigusia jinsi walivyokuwa wameandaa vitanda 1,000 kwenye viwanja vya saba saba jijini Dar es salaam ili kuwalaza lakini kutokana na kupungua kwa wagonjwa, wamesitisha mpango huo.

“Kuna watu walikuwa wanasema (Rais Magufuli) hawakuoni, lakini katika kipindi hiki chenye changamoto, nilikuwa napata maelekezo mengi kutoka kwako. Ukiniona mimi umemwona Rais Magufuli,” amesema Waziri Ummy huku akifurahia pamoja na Rais Magufuli mwenyewe.

Rais John Magufuli

Waziri Ummy amesema, uongozi wa Rais Magufuli umesaidia kuimarisha sekta ya afya na hakuna halmashauri yoyote nchini ambayo haijaguswa ikiwamo ujenzi wa hospitali na vituo vya afya.

Amesema huduma zimeboreshwa ikiwamo kupunguza wagonjwa kupelekwa nje ya Tanzania.

Naye, Rais Magufuli amesema, “waziri wa afya anajituma kweli kweli, katika suala hili la corona alisimama kweli. Kuna wakati fulani nilikuwa namwona kama yuko peke yake kwenye wizara.”

Amesema Waziri Ummy siyo mtaalamu wa afya, wasaidizi wake wote ni wataalamu lakini walimwacha, “nilikutesa kweli. Kuna wakati nilimpigia simu zaidi ya mara nane, hadi uisku. Katika vita, kuna wakati hupaswi kubembelezana.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!