Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Slovenia nchi ya kwanzaUlaya kumaliza corona
Kimataifa

Slovenia nchi ya kwanzaUlaya kumaliza corona

Spread the love

NCHI ya Slovenia, iliyo na watu 2,078,901, wiki hii limekuwa taifa la kwanza barani Ulaya kutangaza hitimisho la maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID-19). Unaripoti mtandao wa habari wa Aljazeera…(endelea).

Msingi wa tangazo hilo, unatokana na Janez Jansa, Waziri Mkuu wa taifa hilo Ijumaa iliyopita kueleza, kusambaa kwa virusi vya corona kumedhibitiwa.

“Leo Slovenia ndio nchi iliyo na hali bora kuhusu janga la corona kwa nchi za Ulaya, hali hii inatuwezesha kueleza kumaliza kabisa janga hili,” amesema Jansa.

Jansa anatoa kauli hiyo ikiwa ni miezi miwili tangi janga hilo kutangazwa ndani ya mipaka hiyo.

Slovenia ni nchi iliyopo Ulaya ya Kati, mashariki mwa milima ya Alpi. Imepakana na Italia, Ghuba ya Adria ya Bahari ya Mediteranea. Mipaka yake inapakana na Kroatia, Hungaria, Italia na Austria.

Serikali ya Slovenia imetangaza, kwamba wananchi wa nchi ya Umoja wa Ulaya (EU) hususani kutoka Italia, Hungaria na Australia, wapo huru kuingia na kupita ndani ya mipaka ya nchi hiyo.

Slovenia imetia mkazo, kwamba raia yeyote wa nje na wale wanaotoka nchi za EU wanaotaka kuingia kwenye taifa hilo, watatakiwa kuwekwa karantini kwa siku 14.

Taarifa za raia wa kwanza wa taifa hilo aliyebainika kuambukizwa virusi vya corona, zilitolewa tarehe 4 Machi 2020, raia huyo alikuwa amerudi nyumbani akitokea Italia.

Kufika tarehe 12 Machi 2020, maeneo mbalimbali ya taifa hilo yaliripoti visa vya corona.

Mpaka kufika tarehe 13 Mei 2020, watu 1,467 ndani ya taifa hilo walikuwa tayari wameambukizwa corona huku vifo vikiwa 103.

“Tangu tulipobaini kuingia na kusambaa kwa virusi vya corona, serikali iliingia kazini kukabiliana na virusi hivyo,” taarifa ya serikali hiyo imeeleza.

Pamoja na taifa hilo barani Ulaya kutangaza kutokuwa na maambukizi mapya, taratibu zilizowekwa wakati wa mapambano dhidi ya corona zimebaki kuwa palepale.

Taratibu hizo ni pamoja na umbali wa zaidi ya mita moja, mikusanyiko mikubwa kutoruhusiwa na uvaaji wa barakoa katika maeneo ya watu wengi.

Mwanzoni mwa wiki hii, Serikali ya Slovenia ilieleza, baadhi ya maduka na hoteli zitafunguliwa wiki ijayo. Pia serikali hiyo imeeleza ligi za taifa lake kurejea tarehe 23 Mei mwaka huu.

Licha ya Slovenia kutangaza kuwa huru dhidi ya virusi vya corona, wataalamu wa afya wa taifa hilo wameeleza, bado virusi vipo ndani ya mipaka hiyo.

“Hakuna taifa lolote Ulaya limetangaza kwamba, limefanikiwa kudhibiti na kumaliza maambukizi mapya ya corona, lakini Slovenia tunapaswa kuwa na tahadhari zaidi,” mtaalamu wa magonjwa ya kuambukizi wa taifa hilo, Mateja Logar alieleza kupitia Televisheni ya taifa hilo jana Jumatano wiki hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!