Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Saratani ya kizazi tishio Tanzania
Afya

Saratani ya kizazi tishio Tanzania

Hospitali ya magonjwa ya Kansa ya Ocean Road
Spread the love

SARATANI ya Mlango wa Kizazi ndio saratani inaoongoza nchini Tanzania kuliko nyingine zinazowakabili binadamu. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea)

Hata hivyo imeelezwa kwa pamoja na kuwa ugonjwa huo unaongoza nchini, bado akina mama hawajawa na mwamko wa kupima afya zao ili kuweza kubaini kuwa wana tatizo hilo au la.

Hayo yameelezwa na Muuguzi kitengo cha uchunguzi wa saratani ya mlango wa Kizazi katika hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Mery Ngowi alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI ONLINE juu ya ukubwa wa tatizo la saRatani ya mlango wa kizazi.

Mery alisema saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama ni kubwa sana nchini kuliko magonjwa mengine ambayo yanatokana na ugonjwa wa saratani.

Hata hivyo, alisema bado akina mama hawajawa na mwamko wa kupima afya zao ili kuweza kubaini kama wanaweza kukumbwa na tatizo hilo ili kuweza kupatiwa matibabu au ushauri ambao unaweza kuwafanya kuepukana na ugonjwa huo.

Muuguzi huyo alisema, katika hospitali ya Benjamini Mkapa walianzisha kitengo cha uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi tangu mwaka 2019  na wamekwisha pokea wagonjwa 95 kati ya hao mmoja alikuwa na mabadiliko ya awali huku 11 wakidhaniwa kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Akizungumzia tatizo hilo alisema, sababu zinazoweza kusababisha kupatikana kwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kuanza kufanya ngono katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuvuta sigara, kuvuta ugoro au kuingiza ugoro katika sehemu za siri pamoja na kujisafisha katika sehemu za siri kwa kutumia sabuni na vitu vyene kemikali.

Aidha alisema, tatizo kubwa la akina mama wengi kutokuwa na mwamko wa kupima saratani ya mlango wa kizazi ni kutokana na kutopata maumivu haraka pindi mtu anapokuwa na maambukizi kwani inaweza kuchukua miaka 10 hadi 15.

Akizungumzia dalili za ugonjwa huo wa saratani ya mlango wa Kizazi alisema ni kutokwa damu mara kwa mara, maumivu chini ya Kitovu na maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Pamoja na hayo Mery alisema kuwa iwapo akina mama watakuwa na mwamko wa kupima afya zao hususani kuwa na mwamko wa kutaka kupima salatani ya mlango wa kizazi ni rahisi zaidi kupatiwa matibabu pale ambapo mgonjwa atakutwa na nabadiliko ya awali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!