Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakati gani mmiliki wa silaha akiua, anakuwa na hatia?
Habari za Siasa

Wakati gani mmiliki wa silaha akiua, anakuwa na hatia?

Spread the love

WIZARA ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania imeeleza, hakuna mazingira yanayomruhusu mmilikiwa wa silaha kuua, na ikitokea hivyo, mahakama itapima. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wizara imetoa kauli hiyo leo Alhamisi tarehe 14 Mei 2020, baada ya Khatibu Said Haji, Mbunge wa Konde visiwani Zanzibar (CUF) kutaka kujua mazingira ambayo anayemiliki silaha anaweza kuua na kutokuwa na hatia.

“Serikali hutoa vibali vya kumiliki Silaha kisheria kwa raia wake kwa ajili ya kujilinda. Je ni wakati gani na matukio gani ya hatari ambayo mmiliki wa silaha anapotumia silaha au hata kuua hatakuwa na hatia?” amehoji.

Katika majibu ya wizara ya mambo ya ndani imesema, silaha itatumiwa na mmiliki wakati wowote kwa matumizi halali yanayozingatia matakwa ya sheria.

Imeeleza, mmiliki wa silaha anaweza kutumia silaha yake katika hali ya kujihami yeye mwenyewe, kumhami mtu mwingine ama mali dhidi ya hatari ama tukio ambalo linaweza kuleta madhara ama athari kubwa dhidi ya maisha au mali.

“Matumizi ya silaha yanayosababisha kifo hayakubaliki kisheria, kwani mmiliki wa silaha anaowajibu wa kutumia silaha kwa usahihi bila kuleta madhara kwa wengine.”

“Hata hivyo, yapo mazingira ambayo mmiliki wa silaha wakati akijilinda ama kumlinda mtu mwingine ama mali, yanaweza kusababisha kifo,” imeeela.

Wizara imesema, “na kwamba, katika mazingira hayo, Mahakama inaweza kupima uwiano wa nguvu iliyotumika ya matumizi ya silaha dhidi ya hatari ama tishio.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!