Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Kabudi atoa sababu Rais Magufuli kutoshiriki vikao vya marais
Habari za Siasa

Profesa Kabudi atoa sababu Rais Magufuli kutoshiriki vikao vya marais

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Spread the love

PROFESA Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, amesema Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC), hajashindwa kufanya majukumu yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Kabudi ametoa taarifa hiyo jana Jumatano tarehe 13 Mei 2020, bungeni jijini Dodoma, baada ya kuibuka mjadala kutoka kwa wabunge waliohoji Rais Magufuli ameshindwa kutekeleza majukumu yake, kama kiongozi wa SADC, kutokana na kushindwa kuitisha mkutano wa jumuiya hiyo.

Hivi karibuni  katika mitandao ya kijamii, yaliibuka madai ya kwamba Rais Magufuli ameshindwa kuitisha mkutano wa SADC, kwa ajili ya kujadili janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19).

Na kwamba, Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini, alichukua hatua ya kuitisha mkutano wa SADC kupitia njia ya mtandao, kwa ajili ya kujadili janga hilo.

Juzi Jumanne tarehe 12 Mei 2020, kulifanyika kikao kingine cha marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) huku Tanzania na Burundi ambazo ni wanachama wa Jumuiya hiyo hazikushiriki kikoa hicho kilichojadilia hatua za kuchukua kujikinga na COVID-19.

Marais walioshiriki kikao hicho kwa njia ya mtandao ni; Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Yoweri Museven (Uganga) na Paul Kagame wa Rwanda ambaye nndiye Mwenyekiti wa EAC.

Akifafanua kuhusu hoja za wabunge, Prof. Kabudi amesema mkutano ule haukuwa wa SADC, bali ulikuwa wa Umoja wa Forodha wa Kusini mwa Afrika (SACU), ambao Tanzania sio mwanachama wake.

Prof. Kabudi amesisitiza kuwa, mkutano ule haukuwa wa SADC, kwa kuwa haukuitishwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo (Rais Magufuli), ambaye ana mamlaka ya kuitisha mikutano kwa kushirikiana na katibu mkuu wa jumuiya hiyo.

Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC akihutubia wajumbe wa mkutano huo

“Kuhusu mkutano wa Rais Ramaphosa, hakuita mkutano wa SADC, mikutano ya SADC inaitishwa na katibu wa SADC kwa kushauriana na mwenyekiti. Ulikuwa wa SACU,  majirani wa Afrika Kusini,” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi alisema, kwa kuwa mkutano huo haukuwa wa SADC, takribani nchi nane mwanachama wa jumuiya hiyo, hazikushiriki. Nchi hizo ni pamoja na: Comoro, Zambia, Malawi, Madagascar, Tanzania, DRC-Congo.

“Akidi ya vikao vya SADC ni 11, na ukimsikiliza Rais Ramaphosa alisema mkutano wa SADC haukuitishwa kwa sababu anayepaswa kuitisha ni katibu wa SADC,” alisema Prof. Kabudi.

Kuhusu madai ya kwamba, Rais Magufuli hajahudhuria mkutano wa EAC, Prof. Kabudi alisema, mkutano huo haukuwa wa EAC, bali ulikuwa wa nchi zinazotumia mtandao wa usafirishaji wa korido ya kaskazini (Northern Corridor ), hivyo nchi ya Tanzania haihusiki na korido hiyo, kwa kuwa iko katika mtandao wa korido ya kati.

“Mkutano ule wa nchi nne ulikuwa mkutano wa pamoja wa  ‘Northern Corridor, lakini sisi na Rwanda tumekuwa na mazungumzo ya ‘Central Croridor, ndio maana sisi na Burundi hatukwenda sababu ni Central Corridor.”

“Ungekuwa wa kwetu, kwanza utafanyikaje bila ya sisi kualikwa, hilo lieleweke na watu wasikuze,” alisema Prof. Kabudi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!