Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy atoa sababu kusitisha taarifa za corona
Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atoa sababu kusitisha taarifa za corona

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema imesimama kutoa takwimu za mwenendo wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19), kwa sababu ya matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza katika maabara inayopima ugonjwa huo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Sababu hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 8 Mei 2020 na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya wa Tanzania, ikiwa zimepita siku tisa tangu Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu, kutangaza ongezeko la wagonjwa wapya 196 wa COVID-19.

Waziri Ummy amesema Serikali itatoa takwimu za mwenendo kuhusu ugonjwa huo, pindi maboresho ya kiufundi katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, yatakapokamilika.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi juu ya ukimya huo, akisema maboresho hayo yatakamilika ndani ya muda mchache.

https://www.youtube.com/watch?v=DACBK6Q0S_c

“Takribani siku saba sasa hatukuweza kutoa taarifa za takwimu za maabara  kuhusu mwenendo wa corona nchini,  kwa sababu sasa hivi tunafanya maboresho  ya  maabara ya taifa ya afya ya jamii.”

“Hivyo niwatoe hofu wananchi kwamba ndani ya siku chache zoezi litakamilika, na tutaendelea kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara,” amesema Waziri Ummy.

Kauli hiyo ya Waziri Ummy ameitoa ikiwa ni siku tano tangu alipomwelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya kuwasimamisha kazi mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dk. Nyambura Moreni na Jacob Lusekelo, Meneja Udhibiti wa Ubora ili kupisha uchunguzi.

Uamuzi huo wa Waziri Ummy ulikwenda sambamba na kuunda kamati ya wataalamu wa afya yenye watu kumi inayoongozwa na Profesa Eligius Lyamuya wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Kamati hiyo inapaswa kukabidhi ripoti kwa Waziri Ummy, tarehe 13 Mei 2020.

Waziri Ummy alitoa maagizo hayo ikiwa ni siku moja kupita tangu Rais wa Tanzania, John Magufuli kubainisha changamoto mbalimbali kwa maabara hiyo ikiwamo kupima vitu mbalimbali ikiwamo mapapai na mbuzi na kukutwa na corona hali aliyodai inaonyesha hakuna umakini katika maabara hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!