Tuesday , 18 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Mhasibu wa AMCOS, wafanyabiashara 16 mikononi mwa Takukuru
Habari Mchanganyiko

Mhasibu wa AMCOS, wafanyabiashara 16 mikononi mwa Takukuru

Spread the love

PAUL Nkuba, Mhasibu wa Chama cha Msingi cha Wakulima wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga, cha MHEDI, pamoja na wafanyabiashara 16, wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao imetolewa leo Ijumaa tarehe 8 Mei 2020 na Emmanuel Stenga, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mwanza.

Stenga amesema Nkuba anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa dawa za kilimo, zenye thamani ya zaidi ya Sh. 12.6 milioni.

Stenga amedai  katika uchunguzi wake, TAKUKURU kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba, imebaini Nkubi anasambaza dawa hizo kwenye maduka binafsi badala ya kuzisambaza kwa wakulima.

“Mhasibu huyo wa AMCOS ya MHEDI maarufu kwa jina la Nchimika, amekuwa akifanya ubadhirifu kwenye usambazaji wa dawa za kilimo za Serikali, zilizonunuliwa kupitia Bodi ya Pamba kwa lengo la kuwapatia wakulima wa pamba kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS),” amesema Stenga na kuongeza:

“TAKUKURU imefanya upekuzi kwenye maduka ya pembejeo za kilimo kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba, baada ya kubaini kuwa dawa za bodi ya pamba zilizoletwa kwa lengo la kuwapatia wakulima kupitia AMCOS zilizopo kwenye maeneo yao, zinauzwa kwenye maduka na wafanyabishara,” amesema Stenga.

Stenga amesema TAKUKURU ilibaini ubadhirifu huo baada ya kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba, hususan ya pembejeo kutowafikia kwa wakati na ucheleweshwaji wa malipo yao baada ya mauzo.

“Baada ya kubaini changamoto hizo, TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa kutambua kwa njini pembejeo za kilimo haziwafikii wakulima kwa wakati, ndipo ilipobaibni kuwa baadhi ya viongozi wa AMCOS wasio waadilifu wamekuwa wakiuza dawa hizo kwa wafanyabiashara wa maduka ya dawa za kilimo,” amesema Stenga.

Wakati huo huo, Stenga amesema TAKUKURU imefuatilia madeni ya wakulima na kufanikiwa kuokoa fedha nyingi zilizohujumiwa na baadhi ya viongozi wa AMCOS mbalimbali jijini Mwanza.

“Baadhi ya viongozi wamekuwa wakizifanyia hujuma fedha za Serikali kwa kuandaa vocha za usambazaji wa pembejeo hewa za kilimo na kuidai fedha nyingi Serikali, kukata kwa wakulima fedha za pembejeo za kilimo na kutoziwasilisha serikalini na kufanya ubadhirifu wa pembejeo za kilimo kwa kuwauzia wafanyabishara badala ya wakulima,” amesema.

Kufuatia changamoto hiyo, Stenga amewaonya wanaohusika na ubadhirifu huo kuacha mara moja, kwa kuwa  zoezi la kuwabaini ni endelevu, na kwamba watakaobainika kuhusika na ubadhirifu wa pembejeo za kilimo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

CoRI: Waandishi wa habari 16,000 hawana mikataba ya ajira Tz

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wachimba chokaa 300 waomba mikopo kuondokana na matumizi ya kuni

Spread the loveKUNDI la vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa chokaa katika kijiji...

error: Content is protected !!