Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DC mwingine afariki dunia Tanzania
Habari za Siasa

DC mwingine afariki dunia Tanzania

Seleman Jafo
Spread the love

HAMIM Gwiyama, Mkuu wa Wilaya (DC) wa Nyang’hwale mkoani Geita amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Rebecca Kwandu, Mkuu wa KItengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais- Tamisemi imemnukuu Waziri wa Tamisemio, Seleman Jafo akitangaza kifo cha Gwiyama kilichotokea leo Alhamisi tarehe 7 Mei 2020 saa 5 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Waziri Jafi amesema DC huyo aliongoza wizara hiyo tangu tarehe 26 Juni 2016 alipoteuliwa na Rais John Pombe Magufuli.

Katika taarifa hiyo, Waziri Jafo amemtumia salamamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel, wananchi wa wilaya hiyo, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo.

Kifo cha Gwiyama kimetokea ikiwa ni takribani siku kumi tangu Evod Mmanda, aliyekuwa

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara  kufariki dunia, tarehe 27 Aprili 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!