Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wenyeviti wa vijiji wawili, mtendaji kata mbaroni Dodoma
Habari Mchanganyiko

Wenyeviti wa vijiji wawili, mtendaji kata mbaroni Dodoma

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania, imewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, wenyeviti  wawili (wa kijiji na kitongoji),  pamoja na afisa mtendaji wa kijiji wa wilayani Chamwino, kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa iliyotolewa kwa umma leo Alhamisi tarehe 7 Mei 2020 na Sosthenes Kibwengo, Mkuu wa TAKUKURU Dodoma imeelezea jinsi wenyeviti hao walivyohusika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kibwengo, Chizenga Masagasi Chimya, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Muungano, Salehe Wistone Chagulula, Mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na Jonas Ivan Nganje, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Iyoyo,  wamefunguliwa Shauri la Jinai Na. 80/2020.

Kibwengo amesema Chimya na Chagulula,  wanatuhumiwa  kuomba na kupokea rushwa ya Shilingi 70,000, ili kuhamisha lalamiko la mwananchi kwenda katika Kituo cha Polisi, ili lifanyiwe kazi.

“TAKUKURU imewafikisha mahakamani Chimya na Chagulula kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo ya Shilingi 70,000, ili waweze kuhamisha lalamiko la mtoa taarifa kwenda polisi kwa hatua zaidi,” amesema Kibwengo.

Kibwengo amesema Nganje ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Iyoyo katika kijiji cha Muungano wilayani humo, alifikishwa mahakamani kwa kosa la kushawishi na kupokea hongo Sh. 25,000, kutoka kwa mwananchi .

Wakati huo huo, TAKUKURU inamshikilia Simon Mapunda Jumbe, Mkazi wa Kisasa jijini Dodoma kwa tuhuma za kujifanya afisa wa taasisi hiyo katika Ikulu ya Chamwisho, na kutapeli zaidi ya Sh. 2 milioni.

Kibwengo amesema Jumbe aliwahi kumtapeli mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kiasi cha Shilingi 2.4 milioni ili amsaidie kupata ajira kama msaidizi wa TAKUKURU , pamoja na mwanamke mmoja kiasi cha Shilingi 214,00.

Pia, Jumbe anadaiwa kumtapeli mwananchi mmoja Sh. 350,000, kwa kigezo cha kumpatia kazi ya udereva katika taasisi hiyo na kumtaka ampe kiasi hicho cha fedha, baada ya kumweleza kwamba hana leseni ya udereva.

“Ufuatiliaji wetu umeonyesha kwamba mtuhumiwa alimwaidi kaka wa mtoa taarifa wetu kazi ya udereva ndani ya TAKUKURU, baada ya mtu huyo kumweleza hana leseni ya udereva daraja C, alimtaka ampe 350,000, ili amsaidie kupata leseni,” amesema Kibwengo.

Kibwengo amesema TAKUKURU inaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo, na kwamba ukikamilika hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.

“Kwa kuwa uchunguzi wetu umebaini kuwa mtuhumiwa amekuwa akifanya utapeli wa aina hii katika maeneo mengi kwa kutumia mbinu mbalimbali, ni vema umma ukamwona na kumtambua ili asiendelee kutapeli watu wengine,” amesema Kibwengo na kuongeza:

“Lakini pia ni fursa kwa wale waliowahi kutapeliwa na mtu huyu kuwasilisha taarifa zake TAKUKURU mkoa wa Dodoma.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!