Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Corona yabadili mwelekeo CCM
Habari za SiasaTangulizi

Corona yabadili mwelekeo CCM

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesitisha shughuli zenye mikusanyiko ya watu wengi, ikiwa ni hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19), unaosababishwa na virusi vya corona. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 17 Machi 2020 na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa.

Amesema, mikutano yote ikiwemo ya ndani na hadhara yenye asili ya mikusanyiko ya watu wengi, itasimama hadi pale chama hicho kitakapotoa maagizo mengine.

“CCM taasisi kubwa, kinazo shughuli zake zinazoendelea kutoka mwanzo hadi mwisho wa mwaka, matukio makubwa ya ujenzi wa chama ya nje na ndani ya jamii.

“Maelekezo shughuli zote za CCM zenye asili ya mikusanyiko mikubwa, iwe ya ndani au ya hadhara. Shughuli hizo zisitishwe mara moja kuanzia leo,” amesema Polepole.

Polepole amesema ziara za viongozi wa chama hicho zilizokua zimeanza au zinazoratarajiwa kufanyika zitasimama kuanzia leo, hadi pale hali itakapokua shwari.

“Ziara za voongozi wa chama zinasimama sasa mpaka tutakapotoa maelekezo mengine sisi kama chama,” amesema Polepole na kuongeza:

“Vikao vya chama ambavyo viko kwenye ratiba ya kalenda, ikiwemo vya halmashauri kuu ya vikao vya kawaida visivyokua na watu wengi chama kitatoa utaratibu wa kufanya.”

Polepole amekosoa uamuzi wa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alioutoa jana tarehe 16 Machi 2020, kwamba wataanza mikutano ya hadhara Aprili mwaka huu.

“Bwana Freeman Mbowe anahamasisha watu kufanya mikutano ya hadhara hapa Watanzania mpime nani anawapenda, nani anataka kuwatumia. Corona inauwa kweli na ukiipata ni rahisi kuambukiza wengine na eneo rahisi kuambukizana ni kwenye mikusanyikon,”  Polepole na kuongeza:

“CCM inapenda mikutano ya hadhara lakini hatutaki kufanya siasa katikati ya hatari inayokabili kwa taifa. Lakini kwa sababu Mbowe masilahi yake sio hayo, anaendelea kuhamasisha watu kufanya mikutano.

“Natoa rai kwa wafusi wa Mbowe wathamini uhai wao kwanza kabla ya kutekeleza agizo la Mbowe. Sababu tiketi rahisi ya kufa ni kwenye mikutano.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!