September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagonjwa wa corona waongezeka nchini, wafikia watatu

Spread the love

WAGONJWA wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-2019) nchini Tanzania wameongezeka kutoka mmoja hadi kufikia watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza tathimini ya hali ya mlipuko huo, Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu, amesema wagonjwa hao wawili ambao ni raia wakigeni, mmoja (Rais wa Ujerumani) yuko visiwani Zanzibar, na mwingine (Rais wa Marekani) yuko jijini Dar es Salaam.

“Tayari wagonjwa wawili wamepatikana, tuna mgonjwa mmoja kutoka Zanzibar, sampuli zake zililetwa maabara kuu ni mjerumani wa miaka 24 amepata maambukizi sasa yuko kwneye uangalizi, Dar es Salaam kuna Mmarekani wa miaka 61, amegundulika na virusi vya Corona. Hivyo tuna ongezeko la wagonwja wawili mmoja wa Zanzibar na Dar es Salaam,” ameeleza Waziri Majaliwa.

Kufuatia mlipuko huo, Waziri Majaliwa amesema vyuo vikuu vitafungwa huku akimuagiza Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu kufanya marekebisho ya ratiba za masomo, ikiwemo za mitihani.

“Vyuo vya ualimu vilitakiwa kufanya mitihani mwezi Mei mwaka huu, naagiza yafanywe marekebisho ya mihula yao,” ameagizwa Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa ameendelea kuwahimiza Watanzania kuepuka mikusanyiko isiyokuwa na lazima. Hata hivyo, amesema shughuli za kijamii ikiwemo kwenye masoko zifanyike kwa tahadhari kubwa ili kujikinga na janga hilo.

“Watanzania tunapaswa  kuwa makini lakini kutokua na taharuki ili kuendelea na shughuli zetu, tunapochukua hatua hizi tunapaswa tathimini ya athari, kusitisha baadhi ya shughuli, kupunguza misongamano na makusanyiko yasiyokua muhimu tubaki, na maeneo muhimu. Shughuli za maduka na masoko zinaendelea, “ amesema Waziri Majaliwa.

Pia, ametoa wito kwa watoa huduma za usafirishaji kuhakikisha hawajazi abiria.

“Huduma za usafirishaji zitaendelea lakini wasafirishaji waelimishe abiria, hakuna haja ya kuwajaza, ili Watanzania   wapate huduma zote za kusafiri, kuhusu wagonjwa tunaendelea kuhifadhi hadi pale tutakapojiridhisha tatizo limekwisha, tuendelee kuwa makini maeneo ya mipaka ili kujiridhisha wote wanaoingia nchini wako salama,” amesema Waziri Majaliwa.

error: Content is protected !!