Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wamdhibiti Zitto Kigoma
Habari za Siasa

Polisi wamdhibiti Zitto Kigoma

Spread the love

JESHI la Polisi wilayani Kigoma limemzuia Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini, kufanya mkutano wake wa hadhara na wananchi, leo tarehe 17 Januari 2020, kwenye Viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na SSP Mayunga Mayunga, Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilayani Kigoma, mkutano huo umezuiwa kwa sababu za kiusalama,  kutokana na taarifa za kiintelijensia ilizopata jeshi hilo.

“Napenda kukujulisha kuwa mkutano huo umezuiliwa kwa tarehe uliyoomba, kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelejensia zilizopo. Kwa hiyo hauruhusiwi kufanya mkutano au kuendelea na maandalizi ya mkutano huo,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Kufutia hatua hiyo, Zitto amesema sababu zilizotolewa na jeshi hilo kuhusu mkutano huo kuzuiwa, hazikuwa za msingi.

“Polisi wamezuia mkutano wetu wa Hadhara wa Mbunge. Jana jioni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini amepata barua hii ya Polisi kuzuia Mkutano halali wa Mbunge kuzungumza na Wananchi wake. Sababu zilizotolewa ni za kipuuzi ‘intelijensia’,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amesema mkutano huo ulilenga kuzungumzia maendeleo ya wananchi wa jimbo lake, pamoja na changamoto ya huduma ya usajili wa vitambulisho vya taifa, inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho nchini (NIDA).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!