Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vurugu zatawala mkutano wa Jiji la Dar es Salaam
Habari za SiasaTangulizi

Vurugu zatawala mkutano wa Jiji la Dar es Salaam

Spread the love

MKUTANO wa Kamati ya Fedha na Uongozi wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, umemalizika baada ya kufanyika chini ya mtutu wa bunduki. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

“Mkutano ule ulikuwa uanze saa 8 mchana, lakini umeanza saa 12 na dakika tano Arasili. Na hapa ni baada ya mkurugenzi kuita polisi na kuendesha kikao kwa njia ya mtutu wa bunduki,” ameeleza Saed Kubenea, mbunge wa Ubungo na mjumbe wa Kamati ya Fedha katika Jiji la Dar es Salaam.

Amesema, “…hivi vinavyoendeshwa hapa haviwezi kuwa vikao vya Jiji kwa mujibu wa kanuni zetu. Vikao vinatakiwa viendeshwe kwa uhuru na kila mjumbe atakuwa na uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuingilia. Linapokuja suala la Polisi kusimamia vikao, hapo hakuna mkutano.”

Kubenea amesema hayo mara baada ya kutoka kwenye kikao hicho ambapo ameleeza kuwa vikao vya aina hiyo, “vimekosa uhalali.”

Amemtuhumu mkuregenzi wa jiji hilo kwa kushindwa kuwa mtumishi wa umma, badala yake ameamua kujiegemeza kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Kubenea, kitendo cha kuita Polisi kinahatarisha mustakabali wa Jiji hilo na kwamba “vikao vya Jiji kuendeshwa na mtutu wa bunduki, ni hatari kwa mustakabali kwa Jiji.”

Amesema, msimamo wake yeye na wenzake, ni kuwa Isaya Mwita ni meya halali wa Jiji na wanaomtaka kumtoa  kwenye nafasi hiyo, wafuate taratibu.

MwanaHALISI Online limeshindwa kumpata mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana, kutoa ufafanuzi wa madai hayo. 

Naye Patrick Assenga, diwani wa Kata ya Tabata na Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya jiji hilo amesema, kikao kilichofanyika kimetia aibu halmashauri hiyo.

Ameeleza kuwa mchakato wa kumtoa kitini Meya Mwita ulikuwa haramu na kwamba hatua ya Meya Isaya kuingia kwenye kikao na kukiendesha ni uthibitisho tosha kuwa meya huyo ndiye mwenye jiji lake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

error: Content is protected !!