Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Meya’ Isaya apata msoto Kisutu
Habari za Siasa

‘Meya’ Isaya apata msoto Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kuzuia madiwani jijini humo, kufanya kkao cha kumuondoa madarakani. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Hii ni mara ya pili kwa mahakama hiyo kuahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Mwita, ambapo jana tarehe 8 Januari 2020, Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Mtega aliahirisha na kueleza angefanya hivyo leo tarehe 9 Januari 2020.

Maombi hayo yaliwasilishwa jana mahamani hapo, siku moja baada ya Sipora Liana, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kutoa wito wa kufanyika kikao hicho.

Kupitia wakili wake – Hekima Mwasipu – Isaya aliomba mahakama kuizuia kikao hicho kujadili ajenda ya kumuondolewa madarakani mpaka pale kesi ya msingi itakaposikilizwa.

Leo tarehe 9 Januari 2020, hakimu Mtega amesema, bado hajaandika uamizi, hivyo ataoa kesho saa tano asubuhi.

Wakati hakimu Mtega akisema hivyo, tayari kikao cha kumng’oa Isaya kimefanyika na kufikia hitimisho la kumuondoa madarakani licha ya akidi ya wajumbe kutokamilika.

Mahakamani hapo, wakili wa serikali Gabriel Malata, aliyewakilisha majabu, aliitaka mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo.

Isaya amehudhuria mahakamani na gari aina ya Raum, ambayo si ile aliyokuwa akiitumia wakati akiwa meya. Gari ya umeya amenyang’anywa leo sambamba na ofisi yake kufungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!