April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askari aliyejitosa kwenye matanki ya mafuta apandishwa cheo

Spread the love

WILSON Mwageni, Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini aliyeonyesha ushujaa baada ya kuingia kwenye eneo lililokuwa na matanki ya mafuta yanayowaka moto amepandishwa cheo. Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salam … (endelea).

Mwageni alifanya tukio hilo jana  usiku tarehe 8 Januari 2020 wakati hifadhi ya mafuta inayomilikiwa na kampuni ya Lake Oil eneo la Vijibweni Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam ilipokuwa ikiteketea kwa moto ambapo alifanikiwa kuingia na kufunga pampu ya mafuta na kuzuia moto usisambae katika maeneo mengine.

Akimtunuku cheo hicho Fikiri Salla, Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andengenye amesema amempandisha cheo askari huyo kutoka Sajenti kuwa Stesheni Sajenti kutokana na akitendo hicho cha ujasili na uzalendo.

“Kamishna Jenerali amenikasimia madaraka aliyonayo kwamba nikucishe cheo hiki na ningependa maafisa na maaskari wengineo mliokuwepo kwenye tukio hilo Kamishna atawapatia vyeti maalum vya ushujaa kwa kufanya kazi kubwa ya jana na kuwa na ushirikiao ikiwemo kituo cha Temeke,Ilala, Kinondoni pamoja na Kibaha.”

“Maafisa na askari muweke moyo wa kujitolea mbele na tufuate mfano wake lakini kubwa Zaidi tufuate tarati bu za kiusalama”

Akizungumzia kitendo hicho cha kupandishwa cheo, Mwageni amesema kuwa hakutegemea kama angepandishwa cheo hicho na kuwa alifanya kwa kuokoa madhara ambayo yangeweza kutokea.

“Sikutegemea, nashukuru mungu kwa hili lililotokea, niliajiriwa kufanya kazi na sio kupewa masharti ya kwamba nitapewa zawadi lakini hayo yote ni ya ziada, napenda kutumia kauli ya Rais kuwa ‘hapa kazi tu’ na nimeifanya kazi,” amesema Mwangeni.

Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo ya moto hakijafahamika na uchunguzi unaendelea na tathmini ya madhara yaliyotokea bado haijajulikana.

Askari huyo wa kikosi cha zimamoto ambaye alifanya kazi hiyo akiwa nje ya muda wake wa kazi huku akiwa amevalia mavazi ya kiraia lakini baada ya kupata taarifa ya moto huo kutokana na kuwa karibu na eneo la tukio akaamua kutoa msaada na alikuwa mtu wa kwanza kabla ya msaada mwengine kujitokeza baada ya kupata taarifa kuwa ili kufanikisha kupunguza madhara inatakiwa ifungwe.

Akisimulia mkasa huo jana muda mfupi baada ya kujitoa muhanga, Mwageni alisema aliambia njia ya kuingilia humo ipo kwa upande wa nyuma ambapo moto huo ulikuwa bado haujawa ndipo alipoamua kumshirikisha kiongozi wake na kumwambia yeye ameamua kujitolea kwa ajili ya nchi yake na ikiwa atapoteza maisha basi watamuombea kwa Mungu.

error: Content is protected !!