October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matokeo kidato cha Pili, Nne haya hapa

Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa Necta

Spread the love

BARAZA la Mitihani nchini (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la nne, Kidato cha Pili na Nne leo tarehe 9 Januari 2020. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Matokeo hayo yametangazwa leo jijini Dodoma na Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa baraza hilo

Darasa la Nne

Amesema, darasa la nne ufaulu wake umeengezeka ambapo jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani 1,531,120, wanafunzi 1,665, 863 wamepata alama A,B,C na D ikilinganishwa na wanafunzi 1,213, 132 waliofaulu wa mwaka 2018.

Matokeo ya darasa la nne haya hapa

Kidato cha Pili

Dk. Msonde amesema, wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya wanafunzi 571,137, wamefaulu na kuingia Kidato cha Tatu.

Matokeo ya kidato cha pili haya hapa

Kidato cha Nne

Amesema, watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722, wamefanya vizuri kwenye mitihani yao.

Matokeo ya kidato cha nne haya hapa

error: Content is protected !!