Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vyama vilivyosusa uchaguzi: Watanzania jiandaeni kujibu mapigo
Habari za SiasaTangulizi

Vyama vilivyosusa uchaguzi: Watanzania jiandaeni kujibu mapigo

Spread the love

VYAMA saba vilivyojitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vimewataka wanachama wake kukaa mkao wa kujibu mapigo, ikiwa mapendezo yao kuhusu uchaguzi huo, hayatafanyiwa kazi na mamlaka husika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Hayo amesema Profesa Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, wakati akisoma tamko la vyama hivyo, leo tarehe 16 Novemba 2019, jijini Dar es Salaam.

Prof. Safari ameeleza kuwa, kwa sasa viongozi wa vyama hivyo pamoja na makundi mengine, wako katika majadiliano kuhusu hatua zitakazochukuliwa na kisha watatoa maelekezo kwa Watanzania ya maazimio ya majadiliano hayo.

“Tunatoa wito kwa Watanzania wapenda demokrasia, wajiandae kwa maelekezo yoyote yatakayotolewa, baada ya mashauriano yanayoendelea miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa na pia makundi mengine ya kijamii,” amesema Prof. Safari.

Miongoni mwa mapendekezo ya vyama hivyo, vinavyotaka yafanyiwe kazi na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ni pamoja na kufutwa kwa uchaguzi huo na kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi.

“Uchaguzi huu ufutwe na mchakato wake uanze upya, kwa mustakabali wa amani ya taifa letu. Tunataka mchakato wa kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi zote nchini, uanze mara moja,” amesema Prof. Safari.

Aidha, vyama hivyo, vimewataka viongozi wastaafu na viongozi wa dini, kuingilia kati suala hilo, ili muafaka upatikane.

“Tumetambua kauli na wito uliotolewa na baadhi ya viongozi wastaafu na viongozi wa dini, hivyo tunawaomba wachukue hatua za kuingilia kati mapema kuinusuru amani ya taifa letu,” amesema Prof. Safari.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika tarehe 24 Novemba 2019, ambapo kampeni zinatarajia kufanyika kuanzia tarehe 17 hadi 23,  Novemba mwaka huu.

Mpaka sasa, vyama vya ACT-Wazalendo, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, UPDP, CCK na NLD, vimetangaza kutoshiriki uchaguzi huo.

Hata hivyo, Serikali imeendelea na msimamo wake wa kwamba uchaguzi huo uko palepale na itafanyika tarehe iliyopangwa, katika maeneo yenye mgombea zaidi ya mmoja.

Na katika maeneo yenye mgombea wa chama kimoja, uchaguzi hautafanyika, na mgombea husika atapita bila kupingwa, kisha kuapishwa na msimamizi msaidizi  wa uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!