October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi watimiza agizo la Mahakama, Halima Mdee mbaroni

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe akiwa mahakamani Kisutu

Spread the love

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe (Chadema) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Oysterbay, kwa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Novemba 2019 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mdee anashikiliwa baada ya kujisalimisha kituoni hapo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Mdee alikwenda katika kituo cha polisi cha Oysterbay, kwa ajili ya kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (RCO).

Hata hivyo, Polisi wamesema watamshikilia Mdee hadi Jumanne ijayo ya tarehe 19 Novemba 2019, watakapomfikisha mahakamani.

Jana tarehe 15 Novemba 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliamuru Mdee pamoja na wabunge wengine watatu wa Chadema, kukamatwa kutokana na kushindwa kufika mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, bila ya kutoa taarifa.

Amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

Wabunge wengine ambao mahakama imeamuru wakamatwe ni Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini.

error: Content is protected !!