Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakiri kuiba Tausi Ikulu
Habari Mchanganyiko

Wakiri kuiba Tausi Ikulu

Spread the love

WATU watatu wamekiri kuiba ndege watatu aina ya Tausi, wanaodaiwa kuwa mali ya serikali – Ikulu, wenye thamani ya Sh. 3,444,150. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, watuhumiwa hao Jumatano tarehe 30 Oktoba 2019 wamekubali kulipa fidia.

Imeripotiwa, washtakiwa hao – Mohamed Ally, David Graha na Mohamed Hatibu – wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai Mosi 2015 na Oktoba 14, 2019, jijini Dar es Salaam.

Licha ya kulipa fidia hiyo, imeamriwa ndege hao warudishwe serikalini. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amesema, washtakiwa hao wamefikia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) tarehe 28 Oktoba 28 2019.

Mpaka sasa, washtakiwa hao wamelipa fidia 6,890,000 kama hasara waliyosababisha, na kwamba adhabu nyingine kwa mujibu wa sheria zitatolewa na mahakama ndipo waachiwe huru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!