WATU watatu wamekiri kuiba ndege watatu aina ya Tausi, wanaodaiwa kuwa mali ya serikali – Ikulu, wenye thamani ya Sh. 3,444,150. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, watuhumiwa hao Jumatano tarehe 30 Oktoba 2019 wamekubali kulipa fidia.
Imeripotiwa, washtakiwa hao – Mohamed Ally, David Graha na Mohamed Hatibu – wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai Mosi 2015 na Oktoba 14, 2019, jijini Dar es Salaam.
Licha ya kulipa fidia hiyo, imeamriwa ndege hao warudishwe serikalini. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amesema, washtakiwa hao wamefikia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) tarehe 28 Oktoba 28 2019.
Mpaka sasa, washtakiwa hao wamelipa fidia 6,890,000 kama hasara waliyosababisha, na kwamba adhabu nyingine kwa mujibu wa sheria zitatolewa na mahakama ndipo waachiwe huru.
Leave a comment