April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai aimwagia sifa Kenya

Bunge la Kenya

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge ameipongeza Kenya kwa kuzindua Kanuni za Kudumu za Bunge lake, kwa lugha ya Kiswahili. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Spika Ndugai ametoa pongezi hizo leo tarehe 31 Oktoba 2019, wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, nchini Kenya.

Aidha, Spika Ndugai amelipongeza Bunge la Kenya kwa hatua ya kuanzisha utaratibu wa kurusha moja kwa moja, matangazo ya vikao vya kamati mbalimbali.

“Nawapongeza kwa uzinduzi, kwamba sasa vikao vya kamati mbalimbali vitapeperushwa mubashara,” amepongeza Spika Ndugai.

Pia amezitaka nchi za Afrika Mashariki kutumia lugha ya Kiswahili katika vikao vyake vya Bunge.

“Nchi zetu kwa muda mrefu zimefunikwa na kasumba ya kuamini kwamba, lugha zetu ni dhaifu na za watawala wetu ni lugha za juu.

“Hatuna sababu za kuwa wanyonge kwa kutumia kiswahili bungeni,” amesema Spika Ndugai.

error: Content is protected !!