Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yaingia ‘Top Ten’ mazingira bora uwekezaji Afrika
Habari Mchanganyiko

Tanzania yaingia ‘Top Ten’ mazingira bora uwekezaji Afrika

Spread the love

TANZANIA imeshika nafasi ya saba, katika nchi 20 zenye mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 28 Oktoba 2019, Geofrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) amesema, utafiti huo huria uliofanywa na Kampuni ya APSA.

Amesema, APSA ni kampuni inayoaminika na wawekezaji kutokana na tafiti zao, na kwamba mwaka huu imetoa tafiti iliyoibeba Tanzania kutoka nafasi ya 15 mwaka jana hadi nafasi ya saba zenye mazingira rafiki ya uwekezaji Afrika.

“Ukilinganisha na mwaka jana tulishika nafasi ya 15, sasa tupo nafasi ya saba kwenye nchi 20 zenyenye mazingira mazuri ya uwekezaji,” amesema.

Amesema, ipo ripoti nyingine ya ‘Doing Business’ iliyofanya na Shirika la Kifedha la Kimataifa (IFC), ambayo ni sehemu ya Benki ya Dunia (WB). Kwenye ripoti hiyo, wameshindanisha nchi mbalimbali duniani kwa kutumia vigezo 11 vinavyoanisha nchi yenye mazingira rahisi kufanya biashara.

Na kwamba, ripoti ya IFC imeangalia nchi 190 kubwa duniani ambapo Tanzania imekuwa nchi ya 141, mwaka jana kwenye idadi hiyo ya mataifa, Tanzania ilishika namba 144.

 Amesema, serikali inafanya juhudi zaidi kuhakisha Tanzania inapanda zaidi kutokana na miradi ya umeme, reli na ujenzi wa miundombinu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!