July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda ‘amkimbia’ Sheikh Alhad

Paul Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hakufika kuhudhuria kongamano maalum la kuelekea uchaguzi, uchumi wa viwanda, amani, mahusiano na ustawi wa taifa kama alivyoalikwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hatua hiyo imemsikitisha Sheikh Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ndio sheikh wa mkoa huo.

Taarifa zaidi zinaeleza, Makonda na wakuu wa wilaya walialikwa kwenye kongamano hilo, lakini hawakuhudhuria bila kutoa udhuru wowote.

Sheikh Alhad ameeleza kusikitishwa na hatua ya viongozi hao wa mkoa ‘kupuuza’ wito huo, na hatimaye kutohuduria bila kuwepo taarifa zao za udhuru.

Akieleza masikitiko yake kwenye hadhara hiyo, Sheikh Alhad amesema, ujumbe wa mwaliko ulifikishwa kwa viongozi hao lakini anashangaa kutowaona.

Hata hivyo, Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMA), amempoza machungu Sheikh Alhad kwamba, ‘kilio’ chake atakifikisha kwa husika.

Sheikh Alhad amemwagiza Waziri Mwita ambaye amemwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwamba, awaeleza viongozi wa serikali wanapowaalika, wawe wanaitikia wito huo kwa kuwa nao (viongozi wa dini) ni sehemu ya msaada kwa amani ya nchi hii.

error: Content is protected !!