Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waimbaji wa muziki wa Injili wafundwa
Habari Mchanganyiko

Waimbaji wa muziki wa Injili wafundwa

Dk. Aron Uliyo, Mwalimu wa Muziki wa Injili (picha ndogo). Picha wanamuziki wa Injili
Spread the love

WATUNZI wa Muziki wa Injili nchini wametakiwa kutunga nyimbo zenye ubunifu na maarifa kwa ajili ya utukufu wa Mungu badala ya kutunga nyimbo za hovyo hovyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbali na kutakiwa kutunga nyimbo zenye ubunifu pia wametakiwa kujua maana na ulimwengu wa kutumia mziki ambao unaendana na wimbo ulioimbwa kwa kuwa uimbaji unagusa viumbe vyote vilivyopo duniani.

Kauli hiyo ilitolewa na mwalimu wa Muziki wa Injili Dk. Aron Uliyo wakati akitoa mafunzo kwenye semina ya waimbaji wa mziki wa Injili juu ya utunzi na utengenezaji wa muziki wa Injili iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa New Dodoma Hotel Jijini hapa.

Mwalimu Uliyo amesema kuwa muziki ni usanii na sanaa, hivyo ni kipaji ambacho kinatakiwa kutumiwa kwa ustadi mkubwa kwa ajili ya kuweza kutunga wimbo na kutengeneza muziki ambao utaweza kuwa jibu kwa wasikilizani.

“Kazi ya sanaa haitaki kukurupuka inaitaji kuwa na utulivu ili unapokuwa umetunga wimbo lazima uwe na maudhuhi ambayo yanaendana na muziki pamoja na uhusika wa kile kinacholengwa.

“Ikumbukwe kuwa kama utakuwa unaimba wimbo wa kusifu ni lazima uoneshe kusifu, usioneshe ni tofauti na mziki kwani kama itachanganywa itakuwa imepoteza maana,” amefafanua Uliyo.

Katika hatua nyingine amesema kuwa muziki ni zawadi kutoka kwa Mungu na uimbaji na mapigo ya mziki yanaanzia tangu mtoto akiwa tumboni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!